Nyumbani » 18/12/2013 Entries posted on “Disemba 18th, 2013”

Maisha ughaibuni si lelemama, yapaswa kujituma na kufanya bidii: Mhamiaji kutoka Tanzania

Kusikiliza / Leo ni siku ya wahamiaji duniani

Ikiwa Disemba 18 ni siku ya wahamiaji duniani, Umoja wa mataifa unataka mazingira bora yawekwe kwa mamilioni ya watu ambao wanahama makwao na kwenda nchi za ugenini kwa sababu zinazotofautiana ikiwemo katika juhudi za kuimarisha maisha yao. Kuna zaidi ya watu milioni 232 waliohama makwao ulimwenguni. Wahamiaji wanapoondoka nchi zao za kuzaliwa wanakumbana na mazingira [...]

18/12/2013 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNMISS yakaribisha kutengamaa kwa hali ya usalama Juba

Kusikiliza / UNMISS

  Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS umesema kuwa umeshuhudia hali kutengamaa kwa kiasi kikubwa mjini Juba leo, na hivyo kuruhusu wafanyakazi wake kuanza tena kutembea mjini asubuhi ya leo. Taarifa kutoka UNMISS imesema ujumbe huo umeanza tena kuweka doria kwa kiwango kidogo mjini Juba, pamoja na kurejesha shughuli za usafiri wa [...]

18/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu la OPCW lapokea ratiba ya kuteketeza silaha za kemikali za SyriaW

Kusikiliza / chemicalweapons

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali, OPCW, Ahmet Üzümcü amewasilisha ratiba ya mpango wa kuteketeza silaha za kemikali zaSyriakwa Baraza Kuu la shirikahilohapo jana. Mpango huo unalenga kutimiza tarehe ya mwisho ilowekwa na Barazahiloya Machi 31 2014 ya kuteketeza silaha hizo, na nyinginezo ifikapo Juni 30 mwakani.   Akilihutubia Barazahilo, Bwana [...]

18/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mauaji ya madaktari Somalia, Mjumbe wa UM alaani vikali

Kusikiliza / Nicholas Kay, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay ameshutumu vikali shambulio la hii leo nje kidogo ya mji mkuu Mogadishu, lililolenga msafara uliokuwa ukielekea kituo kimoja cha afya. Bwana Kay amesema kwenye shambulio hilo lililofanywa na watu wasiofahamika waliokuwa wamejihami, watu sita wameuawa wakiwemo madaktari wanne mmoja ni raia wa [...]

18/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM asema kuwa Korea Kaskazini imetekeleza mauaji ya watu mashuhuri

Kusikiliza / Bendera ya Korea Kaskazini

Mtaalamu wa haki za bindamu kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa kunyongwa kwa  afisa wa ngazi ya juu nchini Korea Kaskazini ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya haki za binadamu. Marzuki Darusman amesema kuwa kukamatwa, kuhukumiwa na kunyongwa kwa Jang Song Thaek mjombake kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ni kitendo ambacho kilifanyika [...]

18/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lajadili ulanguzi wa madawa na amani na usalama Afrika Magharibi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwahutubia wanahabari kuhusu Sudan Kusini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili amani na usalama barani Afrika, hususan suala la ulanguzi wa madawa ya kulevya eneo la Sahel na Afrika Magharibi. Akizungumza wakati wa mkutano huo, Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amesema kote duniani, ulanguzi wa madawa ya kulevya na uhalifu wa kimataifa wa kupangwa hutishia usalama, kudunisha [...]

18/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mpango wa kukwamua uchumi Tanzania waleta nuru kwa kaya maskini: Benki ya dunia

Kusikiliza / Wanawake mkoani Mtwara katika moja ya mikutano ya kuhusu mpango wa kunusuru kaya maskini

Suala la maendeleo na ukuzaji uchumi wenye maslahi ya wengi limeendelea kuwa ni changamoto kwa nchi maskini ikiwemo Tanzania. Benki ya dunia inasema kuwa takwimu za ukuaji wa sekta kama vile kilimo inayogusa wakazi wengi nchini humo ijapokuwa inaonekana kukua lakini bado kaya maskini zinabaki nyuma. Hata hivyo mpango unaotekelezwa nchini Tanzania umeonekana kuwa jawabu [...]

18/12/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uzalishaji wa mbao washuka Ulaya-FAO

Kusikiliza / Bidhaa za mbao

Ripoti  ya shirika la chakula na kilimo FAO imeonyesha kuwa katika msimu wa mwaka 2012 Ulaya haikufanya vyema kwenye soko la kimataifa la mbao huko nchi za Amerika Kusin na Asia –Pacific zikifanya vizuri. Ripoti hiyo mpya imesema sababu kubwa ya Ulaya kufanya vibaya ni matokeo ya mtikisiko wa kiuchumi ulioyaandama mataifa mengine ya Ulaya.Imesema [...]

18/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa waelezea hofu kufuatia ghasia Somalia

Kusikiliza / Askari wa SNA, Somali,AFGOYE Atembea baada ya mvua kubwa

  Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM, Nicholas Kay, ameelezea hofu yake kuhusu machafuko ya hivi karibuni nchini humo. (Taarifa ya Grace) Bwana Kay amesema machafuko yaliibuka katika maeneo kadhaa ya nchi huenda yakatishia barabara ya hatua za kuweka amani na utulivu, pamoja na haki [...]

18/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalam wa UM aitaka Malaysia kutowatenga maskini

Kusikiliza / Umaskini, Malaysia

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za chakula Olivier De Schutter amesema kuwa wakati taifa la Malysia likipiga hatua kuwa taifa lenye kipato cha juu, linapaswa kuhakikisha kwamba mafanikio hayo hayapatikani kwa mgongo wa uharibifu wa mazingira wala mgongo wa makundi ya watu wenye hali ngumu. Akiwa kwenye kilele cha ziara yake [...]

18/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Rider ,Pillay watambua mchango wa wahamiaji duniani

Kusikiliza / Guy Rider, ILO

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kazi duniani ILO  Guy Rider pamoja na Kamishna wa haki za binadamu Navi Pillay  wametoa heshima zao kwa wahamiaji zaidi ya milioni 232 duniani kote ambao kwa nyakati tofauti waliondoka toka maeneo yao ya asili na kwenda sehemu za mbali kwa ajili ya kusaka fursa zaidi. Wakuu hao wamesema kuwa [...]

18/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Afrika Magharibi ina uwezo wa kuimarisha sekta ya kilimo:FAO

Kusikiliza / Soko la mboga, Kerewan, Gambia

Utafiti mpya uliotolewa na shirika la chakula na kilimo FAO  na lile la IFAD umeonyesha kuwa kuimarisha kwa shughuliza za uzalishaji na ushindani pamoja na kuwajengea uwezo wakulima wadogo wadogo ni mambo muhimu yanayoweza kutoa msukumo mkubwa wa kuwa na kilimo hai katika nchi za Afrika Magharibi. George Njogopa na taarifa kamili.  (Taarifa ya George) [...]

18/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNAMID akaribisha hatua ya SLA/Minni Minawi ya kupiga marufuku kuingizwa watoto jeshini.

Kusikiliza / Matumizi ya watooto kama wanajeshi

Mjumbe  maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika kwenye jimbo la Darfur Mohamed Ibn Chambas amekaribisha hatua iliyochukuliwa na kundi la Sudan Liberation Army/Minni Minawi la kusitisha matumizi ya watoto kama wanajeshi. Jason Nyakundi na ripoti kamili. (Ripoti ya Jason)  Bwana Chambas amesema kuwa UNAMID imekaribisha hatua ya kundi la SLA/MM [...]

18/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wanachangia katika kupunguza umaskini: Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Siku ya wahamiaji duniani

Leo ni siku ya kimataifa ya wahamiaji ambapo Umoja wa Mataifa unataka mazingira bora zaidi kwa watu Milioni 232 waliohama makwao na kwenda ugenini kwa sababu mbali mbali ikiwemo kusaka maisha bora.  Joshua Mmali na ripoti kamili. (Ripoti ya Joshua) Uhamiaji wa kimataifa ni njia thabiti ya kupunguza umaskini na kuongeza fursa, na ni jambo [...]

18/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031