Nyumbani » 17/12/2013 Entries posted on “Disemba 17th, 2013”

Baraza la Usalama laelezea hofu kuhusu hali Sudan Kusini

Kusikiliza / Wajumbe wa Baraza la Usalama wakinyoosha mkono kupiga kura

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea kusikitishwa na kuibuka kwa machafuko nchini Sudan Kusini, kufuatia kinachoelezwa kuwa jaribio la kuipindua serikali ya Rais Salvar Kiir. Akizungumza na waandishi wa habari Jumanne jioni mjini New York, rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu, Balozi Gerard Araud wa Ufaransa, amesema "Tunatiwa hofu sana, siyo tu [...]

17/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wazindua mpango wa usaidizi kwa Haiti kwa 2014

Kusikiliza / Mtoto kwenye mojawapo ya kambi za wakimbizi wa ndani nchini Haiti

Huko Geneva, Umoja wa Mataifa umezindua mpango wa mwaka ujao wa usaidizi kwa Haitiwa dola Milioni 169 kwa ajili ya wakazi Laki Nane wa jamii 35 kati ya 140 za nchi hiyo Mwakilishi mkazi wa usaidizi wa kibinadamu nchiniHaiti, Peter de Clercq amewaambia waandishi wa habari kuwa nusu ya fedha hizo ni kwa ajili ya [...]

17/12/2013 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tutaimarisha mafunzo kwa jeshi na polisi Somalia : Kamanda Amisom

Kusikiliza / Kamanda Ntigurirwa

Baada ya kuanza rasmi shughuli zake akiwa kamanda Mkuu wa vikosi vya Afriak nchini Somalia (Amisom), Luteni Ginerali Silas Ntigurirwa ametangaza mipango yake mipya ya kustaawisha taifa la Somalia, ikiwa ni pamoja na kuongoza vikosi vya Amisom na kutafuta vifaa zaidi. Amesema mipango hiyo inachagizwa na dhamira ya kuandaa uchaguzi mkuu mwaka 2016 huku akibainisha [...]

17/12/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNFPA yatoa ripoti ya ubakaji mashariki mwa DRC miezi sita ya kwaza 2013

Kusikiliza / Wanawake DRC

Jimboni Kivu ya kaskazini, zaidi ya vitendo vya ubakaji elfu tatu vilihesabiwa katika mitaa mbalimbali, katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka 2013. Hayo yametangazwa katika ripoti ya wataalam wanao husika na ubakaji, kutoka wizara ya wanawake, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu, UNFPA, ujumbe wa Umoja wa Mataifa [...]

17/12/2013 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Miaka 50 ya uhuru wa Kenya yaenziwa New York

Kusikiliza / Balozi Kamau Macharia na naibu wake Balozi Koki Muli katika sherehe ya miaka 50 tangu Kenya kupata Uhuru, NY

Taifa la Kenya limetimiza miaka 5o tangu lijipatie uhuru wake kutoka kwa wakoloni ,Uingereza. Sherehe za kitaifa zimefanyika nchini humo ambapo wananchi wa taifa hilo lililoko Mashariki mwa Afrika waliadhimisha sherehe hizo kwa mambo kadhaa ikiwamo mkesha maalum ulioshuhudia kupandisha tena bendera ya Kenya kitendo kilichofanyika baada ya kuishusha ya mkoloni. Hapa mjini New York [...]

17/12/2013 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Biashara baina ya nchi zinazoendelea yaongezeka: UNCTAD

Kusikiliza / UNCTAD

Biashara ya bidhaa nchi za nje imeongezeka mara tatu duniani katika miongo miwili iliyopita na kufikia zaidi ya dola Bilioni 18 huku asilimia 25 ya kiwango hicho kikitoka nchi za kusini au zinazoendelea. Hiyo ni kwa mujibu wa kijarida cha takwimu kutoka kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa kilichotolewa leo. Kijarida hicho [...]

17/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakutana kuhusu hali nchini Afghanistan

Kusikiliza / Baraza la Usalama, kikao

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili hali nchini Afghanistan katika muktadha wa amani na usalama wa kimataifa. Joshua Mmali na taarifa kamili. (Taarifa ya Joshua) Mkutano huo wa Baraza la Usalama umehutubiwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA, Jan Kubis ambaye [...]

17/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mswada wa 'NGO' Sudan Kusini watishia huduma za mashirika ya kiraia: Wataalam wa UM

Kusikiliza / kambi nchini Sudan Kusini

    Wataalam watatu maalumu wa Umoja wa Mataifa, leo wameonya kuwa mswada unaojadiliwa sasa na bunge la Sudan Kusini kuhusu mashirika yasiyo ya kiserikali, au NGOs, unatishia kazi na uhuru wa mashirika ya kiraia nchini humo. Wataalam hao wamesisitiza kuwa kipengee cha uangalizi wa serikali kilichopendekezwa katika mswada huo kinavuka mpaka na kuzidi haja [...]

17/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ndege yenye misaada ya kiutu yawasili Bangui

Kusikiliza / Ngege kutoka UNICEF iliyosheheni misaada yawasili Bangui, CAR

Ndege ya mizigo kwa ajili ya kutoa huduma za misaada ya kibinadamu kwa mamia ya raia walioathirika na machafuko yanayoendelea Jamhuri ya Afrika ya Kati imewasili leo Mjini Bangui ikiwa imesheheni tani 77 za huduma mbalimbali. Kuwasili kwa ndege hiyo ya misaada kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kumekuja katika kipindi [...]

17/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Visa vya homa ya kirusi cha korona vyaripotiwa nchini Saudi Arabia

Kusikiliza / Mtaalamu kwenye maabara

  Shirika la afya duniani WHO limefahamishwa kuhusu visa viwili vya homa ya kirusi cha korona nchini Saudi Arabia Kisa cha kwanza kinamhusu mama mwenye miaka 51 kutoka nchini Saudi Arabia  aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo mnamo tarehe 20 mwezi Novemba mwaka huu. Mama huyo alionekana kuwa mgonjwa na baadaye akasafirishwa kwenda Riyadh [...]

17/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban azungumza na Kiir; ataka vikosi vya usalama vizingatie sheria za kimataifa za kibinadamu

Kusikiliza / Polisi wa UM akisaidia wanawake waliokwenda kusaka hifadhi kwenye ofisi za UNMISS  huko Juba. (UNMISS)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini kuhusu mapigano yaliyoanza mwishoni mwa wiki nchini humo na kusababisha sinforahamu ikiwemo raia kusaka hifadhi kwenye ofisi za Umoja huo mjiniJuba. Bwana Ban ameeleza wasiwasi wake juu ya ripoti ya mapigano kati ya [...]

17/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNHCR yapeleka wahudumu zaidi wa dharura CAR

Kusikiliza / Wakimbizi wa CAR katika uwanja wa ndege wa Bangui walikokimbilia baada ya ghasia

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limesema linapeleka timu za ziada za wahudumu wa kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kufuatia kuzorota kwa hali huko na ripoti za watu kulazimika kuhama upya. Jason Nyakundi na taarifa kamili (Taarifa ya Jason Nyakundi) Kulingana na UNHCR, wahudumu hao wameanza kuwasili wiki hii, na wengine [...]

17/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Brahimi asema pande za Syria tu ndio zitashiriki mashauriano

Kusikiliza / Khawla Mattar, msemaji wa mjumbe wa pamoja wa UM na Umoja wa nchi za kiarabu kuhusu mzozo wa Syria, Lakhdar Brahimi

Baada ya tarehe ya mkutano wa pili wa kimataifa wa amani kuhusu Syria kutangazwa kuwa utafanyika tarehe 22 mwezi Januari kwenye jiji la Montreaux nchini Uswisi, hii leo mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu kwenye suala hilo Lakhdar Brahimi amefafanua kile kitakachofanyika. Taarifa zaidi na George Njogopa. (Taarifa [...]

17/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatimaye Fao yawapatia mbegu wakulima huko Ufilipino

Kusikiliza / Wakulima wakipatiwa mbegu kwa ajili ya kilimo. (FAO)

Mwezi mmoja baada ya kimbunga Haiyan kupiga nchini Ufilipino, shirika la kilimo na chakula duniani, FAO limewapatia mbegu wakulima wa kisiwa cha Visayan ambao walipoteza mazaoyaona vifaa vingine muhimu baada ya janga hilo. Tayari usambazaji wa mbegu hizo muhimu umeanza ambapo FAO na idara ya kilimo Ufilipino wanawapatia wakulima mbegu kwa ajili ya kilimo cha [...]

17/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamanda mpya wa AMISOM ataka azimio la Baraza la Usalama litekelezwa haraka

Kusikiliza / Luteni Jenerali Guti na Luteni Jenerali Ntigurirwa wakisalimiana baada ya makabidhiano. (AMISOM)

Kamanda mpya wa kikosi cha Afrika nchini Somalia, AMISOM Luteni Jenerali Silas Ntigurirwa kutoka Burundi ameomba kutekelezwa haraka iwezekanavyo azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linaloongeza idadi ya askari wa kikosi hicho. Amesema hayo punde baada ya kukabidhiwa jukumuhilorasmi mjiniMogadishu, huku akigusia pia ombi la usaidizi wa vifaa. (Sauti ya Luteni Jenerali [...]

17/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031