Nyumbani » 13/12/2013 Entries posted on “Disemba 13th, 2013”

Ban ahutubia Baraza la Usalama kuhusu ripoti ya silaha za kemikali Syria

Kusikiliza / Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-mooon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amelihutubia Baraza Kuu kuhusu ripoti ya uchunguzi katika madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria, kufuatia kukabidhiwa ripoti hiyo hapo jana na Profesa Åke Sellström, ambaye aliiongoza timu ya uchunguzi huo. Ripoti hiyo inajumuisha matokeo ya uchunguzi wote wa timu hiyo katika matukio yote [...]

13/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Haki za binadamu zaenziwa Somalia na Afghanistan

Kusikiliza / Siku ya haki za binadamu, Somalia

Wakati dunia ikiwa imeadhimisha siku ya haki za binadamu mapema wiki hii, utekelezaji wa haki za binadamu katika nchi mbalimbali unakabiliwa na changamoto kadhaa. Hata hivyo kuna juhudi za makusudi za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutekeleza haki hizo. Mathalani Somalia na Afghanistan zimeonyesha nuru na matumaini. Basi ungana na Joseph Msami katika makala [...]

13/12/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Malkia Maxima ashuhudia usaidizi wa wakulima wadogo Dodoma, Tanzania

Kusikiliza / Malkia Maxima wa Uholanzi

Malkia Maxima wa Uholanzi ambaye ni Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ujumuishwaji wa mifumo ya fedha kwa maendeleo,  amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini Tanzania ambayo pia aliambatana na viongozi waandamizi wa umoja huo akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP. Wakati wa ziara hiyo Malkia [...]

13/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baada ya M23 sasa ni vikundi vingine vyenye silaha: UM

Kusikiliza / Herve Ladsous akiwa zairani Pinga Kivu Kaskazini

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa Herve Ladsous amesema baada ya utiwaji saini wa makubaliano ya amani ya Kampala kati ya serikali na kundi la waasi wa M23 yanayotarajiwa kuleta matumaini ya amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC ,sasa ni wakati wa kushughulikia vikundi vingine. Akiongea na [...]

13/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama latakiwa kuchukua hatua kulinda waandishi wa habari mashakani

Kusikiliza / Madhila ya waandishi wa habari

Baraza la usalama leo limeelezwa bayana madhila wanayokumbana nayo waandishi wa habari pindi wanapotekeleza majukumu yao na limetakiwa kuchukua hatua kuhakikisha wanalindwa dhidi ya vitendo hivyo. Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, Frank La Rue amelimbia baraza hilo wakati wa kikao maalum kuhusu ulinzi wa waandishi wa habari [...]

13/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Bahama yatakiwa kuwa na mkakati wa kitaifa wa kupambana na usafirishaji wa binadamu

Kusikiliza / Joy Ngozi Ezeilo

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu usafirishaji wa binadamu Joy Ngozi Ezeilo ameitaka jumuiya ya Commonwealth ya Bahama kuendeleza na kutekeleza haraka mpango wa kitaifa wa haki za binadamu na unaozingatia waathirika ukilenga kupinga ukuaji wa usafirishaji wa binadamu.   Akiongea baada ya kufanya ziara nchini humo Bi Ezeilo amesema Bahama imedhihirisha utayari wa [...]

13/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban aweka bayana mshikamano na wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Salaamu, mimi ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon.. ndivyo alivyoanza Bwana Ban ujumbe wake kwa watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, wakati huu ambapo ghasia zinaendelea nchini humo huko na kuweka maisha ya wananchi hatarini. Ujumbe huo kwa njia ya radio ni takribani dakika mbili ambapo Katibu Mkuu ameamua kuzungumza moja [...]

13/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukatili wa kijinsia wamulikwa nchini Tanzania

Kusikiliza / Ukatili wa kijinsia lazima ukomeshwe

Hatimaye siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizoanza tarehe 25 mwezi uliopita, zimehitimishwa wiki hii ya tarehe 11 Disemba. Katika kipindi hicho harakati mbali mbali zilitekelezwa kupazia sauti mbinu za kutokomeza ukatili wa kijinsia, majumbani, sehemu za kazi, shuleni na kwingineko ili dunia pawe sehemu bora ya ustawi kwa kila mtu bila kujali  jinsi [...]

13/12/2013 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Benki ya dunia yataja miradi ya kunufaisha wakazi wa Goma huko DR Congo

Kusikiliza / Eustache Uoayoro, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia nchini DR Congo

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia huko Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo, DRC Eustache Uoayoro amesema jimbo la kivu ya kaskazini litanufaika na miradi ya maendeleo ya kijamii kwa lengo la kuleta majibu ya haraka kwa matatizo ya wakazi wa jimbohilowaliokumbwa na ghasia za mara kwa mara. Bwana Uaoyoro amemweleza Sifa Maguru wa Radio washirika Okapi [...]

13/12/2013 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha kumalizika kwa mazungumzo baina ya Dr Congo na M23:

Kusikiliza / Waasi wa M23

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban  Ki-moon  amekkaribisha kuhitimishwa kwa majadiliano yaKampalabaina ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokasia yaCongona kundi la M23 kwa kutia saini azimio mjini Nairobi Kenya siku ya Alhamisi. Na pia kutolewa tamko la mwisho na Rais Yoweri Museveni waUgandana Rais Joyce Banda waMalawi, ambao walikuwa wenyeviti wa mkutano wa kimataifa [...]

13/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

CERF ni mkombozi wa wahitaji, twaomba mchangie kuokoa wahitaji: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM, Ban Ki-moon

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na uratibu wa masuala ya usaidizi wa kibinadamu, OCHA leo imeandaa mkutano wa ngazi ya juu kuhusu mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa, CERF mjini New York. Assumpta Massoi amefuatilia mkutano huo na hii hapa ni ripoti yake. (Ripoti ya Assumpta) Mwaka huu pekee CERF ilitoa zaidi ya [...]

13/12/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Elimu kwa watoto nchini Syria yazidi kudorora: UM na wadau

Kusikiliza / Watoto wa Syria, elimu yao sasa imekumbwa na sintofahamu kutokana na mzozo

Shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ,UNICEF Kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kuhudumia watoto, Save the children, World Vision na shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizizi UNHCR wamezindua ripoti hii leo inayohusu mkwamo wa kielimu unaowakumba watoto wa Syria kutokana na mgogoro. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya (Ripoti ya Grace) [...]

13/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tamasha lafanywa kuwakumbuka wahamiaji walokufa maji Mediterranean:IOM

Kusikiliza / Boti zinazotumiwa kuvuka mpaka kupitia Mediterenia

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM ofisi ya Roma Italia pamoja na kwanya ya Roman Philharmonic Orchestra wameandaa tamasha linalofanyika usiku wa leo kwa ajili ya kuwakumbuka wahamiaji waliopoteza maisha Lampedusa katika bahari ya Mediterranian na kwingineko kwa ajili ya kusaka maisha bora. Tamasha hilo litakalofanyika Santa Maria del Popolo Basilica litahudhuriwa pia na mkurugenzi [...]

13/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

MONUSCO kuinua ustawi wa raia DRC

Kusikiliza / Wakazi wa Pinga Kivu Kaskazini wanauza bidhaa sokoni wakati hali ya kawaida ikirejea kufuatia ulinzi wa MONUSCO

Naibu Mwakilishi maalum wa ujumbe wa kuweka utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO, Moustapha Soumaré , ambaye pia ni Mratibu Mkazi wa masuala ya kibinadamu na Mkuu wa UNDP nchini humo, amehitimisha ziara yake ya siku mbili mjini Goma hapo jana Alhamisi. Mwishoni mwa ziara hiyo, Bwana Soumaré  amesema, ziara hiyo ya ujumbe [...]

13/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yasambaza mafuta kwa Wasyria kunapoanza msimu wa baridi

Kusikiliza / Mtoto wa Syria

Huku watu nchini Syria wakikabiliana na msimu wa baridi kali shirika la mpango wa  chakula duniani WFP limeanza shughuli  za usambazaji wa karibu tani 10,000 za mafuta kwa wakimbizi wa ndani wanaoishi kwenye maeneo kumi ya mji wa Damascus. Mafuta yanayosambaza nayo  yatatumika kwenye upishi  na kwa kupasha joto. Usambazaji zaidi wa mafuta unapangwa kufanywa [...]

13/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watu 159,000 walazimika kuhama makwao huku 600 wakiuawa kwenye Jamhuri Afrika ya Aya Kati

Kusikiliza / Watu waliokimbilia kanisani kutoroka mapigano

Mapigano yanayoendelea kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati yamewalazimu karibu watu 159,000  kuhama makwao kwenye mji mkuu Bangui huku watu 450 wakiripotiwa kuawa na wengine 160 sehemu tofauti za nchi kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu na baraza la wakimbizi la Denmark. Kwenye uwanja wa ndege mjini Bangui kuna watu 38,000 wasio na choo [...]

13/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF yasafirisha tani 77 za misaada kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / UNICEF yafikisha msaada CAR

Wiki moja baada ya makabiliano makali yaliyosababisha vifo vya mamia ya watu na wengine mengi kuhama makwao kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati  msaada mkubwa wa kibinadamu umewasili hii leo mjini Bangui kwa njia ya ndege ikiwa imesheheni tani 77 ya misaada kutoka kwa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa  Mataifa [...]

13/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ingawa usalama umeanza kuimarika mvutano wa kidini unatia hofu:UM

Kusikiliza / nembo

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa inasema ingawa hali ya usalama imeanza kuimarika katika siku za karibuni katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Bangui, bado inatiwa hofu na ongezeko la mivutano miongoni mwa jamii za  kidini. Ofisi hiyo inasema mashambulizi kati ya jamii za Wakristo na Waislamu yanaripotiwa kutokea [...]

13/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031