Nyumbani » 11/12/2013 Entries posted on “Disemba 11th, 2013”

Waathirika wa mzozo wa Darfur wamepoteza matumaini: ICC

Kusikiliza / Fatou Bensouda azungumzia Sudan

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Fatou Bensouda, ameliambia Baraza la Usalama leo kuwa, ingawa Baraza hilo lilipitisha azimio 1593 la kuipeleka kesi dhidi ya Rais Omar al Bashir wa Sudan na wengine kwa mahakama ya ICC na kutoa matumaini kwa waathiriwa wa mgogoro wa Darfur, inahuzunisha kuwa matumaini hayo yamezama. [...]

11/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mustakhbali wa uchaguzi Bangladesh, tumieni mashauriano: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon kwenye simu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina pamoja na Rais Abdul Hamid na kuwasihi wapatie suluhu tofauti zinazoibua ghasia nchini humo wakati huu wa kueleka uchaguzi wa wabunge mwezi Januari mwakani. Ghasia hizo zinazozidi kuenea tangu mwezi uliopita zimesababisha vifo. Mazungumzo hayo [...]

11/12/2013 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

M23 tumeshawang'oa, sasa ni FDLR, asema Kobler kwa Baraza la Usalama

Kusikiliza / Walinda amani wa MONUSCO, DRC

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa kuweka utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO, Martin Kobler, ametangaza kuwa baada ya kuwang'oa waasi wa M23 Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, sasa mapambano yanawageukia waasi wa FDLR.   Hayo yamesemwa na rais wa Baraza la Usalama mwezi huu, Balozi Gerard [...]

11/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ni wakati wa watu ukanda wa Maziwa Makuu kufurahia amani: Bi Robinson

Kusikiliza / Mwakilishi maalum  wa Katibu Mkuu wa UM kwenye Ukanda wa maziwa makuu, Mary Robinson

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukanda wa Maziwa Makuu, Bi Mary Robinson, amesema kuwa huu ndio wakati wa kutimiza ahadi zilizowekwa katika makubaliano ya amani, usalama na ushirikiano, ambayo yalisainiwa mjiini Addis Ababa mapema mwaka huu, ili watu wa ukanda wa Maziwa Makuu wapate kufurahia amani. Bi Robinson amesema hayo katika mkutano na waandishi [...]

11/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Juhudi za kunusuru misitu Uganda zaanza

Kusikiliza / Uharibifu wa misitu, msitu wa Kandanda Ngobya, Uganda

Uharibifu wa misitu nchini Uganda katika wilaya ya Hoima sasa ni dhahiri lakini hatua za kunusuru misitu zinachukuliwa mathalani kuanzishwa kwa mradi wa miaka mitatu wa utunzaji wa misitu nchini humo. Juhudi hizi zinazofanywa na asasi za kiraia hapana shaka zinahitaji kuungwa mkono na serikali na jamii kwa ujumla ili kutimiza lengo la mileni la [...]

11/12/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Suala la jinsia bado lina umuhimu kwenye usajili wa watoto: UNICEF

Kusikiliza / Mama akimsajili mwanae kwenye kituo cha usajili vizazi

Suala la jinsia limeelezwa kuwa na umuhimu mkubwa kwenye usajili wa watoto pindi wanapozaliwa kwani katika nchi nyingi uwepo wa baba unarahisisha mtoto kusajiliwa na kupata cheti. Mtakwimu kutoka shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Claudia Cappa amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini New York, kuhusu ripoti ya shirika [...]

11/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watu zaidi ya laki moja wamekufa mgogoro wa Syria ukifikisha siku 1000:UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria waliofurushwa kufuatia mzozo unaoshudiwa Syria

Zikiwa zimetimia siku 1000 tangu mgogoro wa Syria uibuke inaelezwa zaidi ya watu laki moja wamekufa ikiwa ni wastani wa watu mia kwa siku huku wafanyakazi wa misaada na waandishi wa habari wakikabiliwa na vikwazo vya kuwafikia robo ya watu milioni walioko katika maeneo yaliyozingirwa na vikosi. Hiyo ni kauli ya mjumbe maalum wa shirika [...]

11/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mtaalam wa UM wapongeza kuachiliwa kwa wafungwa Myanmar

Kusikiliza / Tomás Ojea Quintana

Mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Myanmar, Tomás Ojea Quintana, amekaribisha kuachiwa huru kwa wafungwa 44 wa kisiasa nchini humo. Mtaalam huyo huru amesema kuachiwa huru kwa wafungwa hao ni hatua muhimu katika kuona kuwa wafungwa wote wa kisiasa wameachiwa huru ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Ameongeza kuwa [...]

11/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Usajili wa watoto wachanga bado ni changamoto: Tanzania yachukua hatua: UNICEF

Kusikiliza / Mtoto akionyesha cheti chake cha kuzaliwa baada ya kusajliwa

Wakati linatimiza miaka 67 tangu kuanzishwa kwake, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema usajili wa watoto wanapozaliwa umesalia tatizo kubwa duniani ambapo takwimu zinaonyesha kuwa watoto Milioni 230 duniani kote hawajasajiliwa popote. Takwimu hizo zimo kwenye ripoti iliyotolewa leo wakati wa maadhimisho hayo iitwayo, Haki ya kila mtoto anayezaliwa: tofauti na [...]

11/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

FAO yataka usaidizi zaidi kwa kilimo cha milimani

Kusikiliza / Akina mama wa vijijini Mashariki ya kati Nepal wakibebe kuni kutoka msitu karibu na makazi yao milimani

Wakati dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya milima hii leo, Shirika la chakula la kilimo duniani, FAO limesema familia za wakulima zinazoishi kwenye milima na kando kando ya milima ni mtaji tosha unaoweza kuboresha hali ya usalama wa chakula na mazingira ya eneohilo.  George Njogopa na taarifa kamili  (Ripoti ya George) Kulingana na ripoti ya [...]

11/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua za kukabiliana na ukwepaji wa sheria nchini DRC zahitaji kuboreshwa: UM

Kusikiliza / Kampeni ya uchaguzi DRC(Picha ya MONUSCO)

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo imebaini kuwa mamlaka nchini DR Congo zimechukua hatua kuwajibisha wakiukwaji wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi mwaka 2011,  lakini hata hivyo mengi hayajafanywa. Jason Nyakundi na taarifa kamili. (TAARIFA YA JASON NYAKUNDI) Ripoti hiyo inataka kuchukuliwa kwa hatua kuhakikisha kuwa uchaguzi ulio mbeleni umefanyika kwenye [...]

11/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa ajira wa muda mrefu ni changamoto kwa nchi nyingi: ILO

Kusikiliza / Ukosefu wa ajira

Wale wanaotafuta ajira wanakumbwa na wakati mgumu wa kupata kazi kwa kipindi cha miezi sita  kwa mujibu wa ripoti mpya y shirika la kazi duniani ILO. Grace Kaneiya na maelezo zaidi.  (TAARIFA YA GRACE KANEIYA) Kipindi cha kutokuwa na kazi kwa wafanyikazi wengine kimekuwa kirefu kwa nchi zingine ikilinganishwa na mwka 2008. Kwa mfano nchini [...]

11/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Harakati dhidi ya Malaria zaonyesha mafanikio makubwa: Ripoti

Kusikiliza / Watoto chini ya vyandarua vya kuzuia mbu

Shirika la afya duniani, WHO leo limetoa ripoti ya mwaka huu kuhusu Malaria inayoonyesha kuwa  juhudi za pamoja za kukabiliana na ugonjwa huo tangu mwaka 2000 zimezaa matunda zikiokoa maisha ya watu milioni 3.3. Ripoti hiyo inasema vifo vitokanavyo na malaria vimepungua kwa asilimia 45 duniani huku barani afrika pekee idadi yake ikipungua kwa asilimia [...]

11/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres atoa ombi la kusaidia wakimbizi wa ndani:UNHCR

Kusikiliza / Mapigano nchini CAR yamefurusha zaidi ya watu nusu milioni mwaka jana

Kamishina mkuu wa wakimbizi Antonio Guterres leo amefungua mjadala wa kila mwaka wa changamoto za kulinda wakimbizi kwa ombi la kuimarisha mtazamo wa kimataifa kwa ajili ya watu takribani milioni 30 duniani ambao wamelazimika kuwa wakimbizi wa ndani nchini mwao. Katika hotuba yake ya ufunguzi mjini Geneva bwana Guterres ameonya kwamba wakimbizi wa ndani wanaongezeka [...]

11/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031