Nyumbani » 10/12/2013 Entries posted on “Disemba 10th, 2013”

Miaka 65 tangu tamko la haki za binadamu, bado haki zinabinywa: Eliasson

Kusikiliza / Naibu Katibu Mkuu wa UM Jan Eliasson

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao maalum kuhusu haki za binadamu kikiangazia mustakhbali wa sualahiloikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki za  binadamu. Wakati wa kikao hicho Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson alieleza bayana kuwa miaka 65 tangu kupitishwa kwa tamko la kimataifa [...]

10/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Global Fund yazitaka serikali kuondoa vikwazo vya haki za binadamu:

Nembo ya global fund

  Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya haki za binadamu , mfuko wa kimataifa wa kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria Global Fund umetoa ombi maalumu kwa la kuondoa vikwazo vyote vya haki za binadamu katika nyanja ya afya, ambavyo ni kizingiti kikubwa katika lengo la kutokomeza ukimwi, kifua kikuu na malaria. Global Fund, [...]

10/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Pillay aisihi Bangladesh kusitisha adhabu ya kunyongwa dhidi ya Mollah

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa haki za Binadamu Navi Pillay amemsihi Waziri Mkuu waBangladeshSheikh Hasina kuagiza kusitishwa kwa adhabu ya kunyongwa dhidi ya mwanaharakati wa kisiasa nchini humo Abdul Quader Mollah aliyepatikana na hatia ya uhalifu wa kivita katika kesi inayodaiwa kutokidhi viwango vya kimataifa. Ombi la Bi. Pillay limo katika barua yake kwa Waziri Mkuu Hasina [...]

10/12/2013 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kiwango cha uelewa wa haki za binadamu chazidi kuongezeka

Kusikiliza / Siku ya haki za binadamu

Tarehe 10 Disemba ni siku ya kimataifa ya haki za binadamu. Siku hii inaturejeshwa mwaka 1948 tamko la haki za binadamu lilipopitishwa na pia mkutano waVienna, uliohusisha pia kuanzishwa kwa ofisi ya umoja wa Mataifa ya haki za binadamu. Haki zote zinaangaziwa ikiwemo ya kuishi, afya, ajira, kumilikimalina hata kuhakikisha wakazi wa dunia hii wanaishi [...]

10/12/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Shamshad Akhtar wa Pakistan kuwa Mkuu wa ESCAP

Kusikiliza / Shamshad Akhtar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Bi Shamshad Akhtar wa Pakistan kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kiuchumi na Kijamii ya Asia na Pasifiki, ESCAP. Bi Akhtar atachukuwa mahala pa Bi Noeleen Heyzer wa Singapore, ambaye Ban amemshukuru kwa mchango wake wa kujitoa kwa ESCAP na kwa ukanda wa Asia na Pasifiki [...]

10/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vikwazo dhidi ya mali za Taylor vyaendelezwa; Somalia yahitaji bado usaidizi

Kusikiliza / Mkuu wa UNSOM, Balozi Nicholas Kay akihutubia Baraza la Usalama kwa njia ya Video kutoka Mogadishu

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo kwa kauli moja limepitisha azimio linalokariri azimio lake la awali linalomzuia Rais wa zamani wa Liberia John Taylor, familia yake na maafisa waandamizi kutumia fedha walizozipata kinyume cha sheria wakati wa uongozi wake. Rais wa Baraza la usalama kwa mwezi huu wa Disemba, Balozi Gerard Araud wa [...]

10/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa UM wahofia hatma ya wafungwa wa Guantánamo

Kusikiliza / Nembo ya Umoja wa Mataifa

Wataalamu maalumu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameelezea kushangazwa na kuhamishwa kwa Djamel Ameziane kutoka Guantánamo Bay kwenda Algeria, huku wakitaja kuhofia hatma ya wafungwa wanaoshukiwa kushiriki ugaidi katika gereza hilo la Guantánamo Bay. Wataalamu hao, Juan E. Méndez anayehusika na utesaji na Ben Emmerson anayehusika na haki za binadamu na vita [...]

10/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Msaada wa dharura wa chakula wawafikia wahitaji CAR:WFP

Kusikiliza / Kituo cha usambazaji wa chakula, CAR

Tathimini ya pamoja nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) imebaini kwamba ghasia zilizozuka upya Desemba 5 mwaka huu zimewatawanya watu zaidi ya 60,000 na chakula ni suala lililo msitari wa mbele kwao.  Na kwa kutambua hilokatika kukabiliana na mahitaji muhimu ya haraka shirika wa mpango wa chakula WFP linatoa msaada kwa waathirika kwenye mji [...]

10/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

AMISOM yaahidi kulinda haki za watu Somalia

Kusikiliza / Balozi Mahamat Annadif na walinda amani wa AMISOM alipozuru sector III

Mjumbe maalumu wa mwenyekiti wa kamishna ya Afrika kwa Somalia amerejelea wito wa kuendelea kuinga mkono taifahilo laSomalia katika wakati ambapo dunia ikiadhimisha siku ya haki za binadamu. Akizungumza sambamba na maadhimisho ya siku hiyo Balozi Mahamat Saleh Annadif amesema kuwa ujumbe wa kimatafa nchini Somalia AMISON umedhamiria kuendelea kuisadia Somalia na kutetea haki za [...]

10/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yaanza operesheni ya kuyang'oa makundi yenye silaha DRC

Kusikiliza / Walinda amani wa MONUSCO wapiga doria Pinga Kivu Kaskazini

Brigedi maalum ya kijeshi ya Ujumbe wa Kuweka Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, MONUSCO ilianza jana operesheni dhidi ya wapiganaji wa FDLR katika eneo la Kalembe, umbali wa zaidi ya kilomita mia moja kaskazini ya Goma, mashariki mwa DRC. Hayo yametangazwa Jumanne na kamanda wa majeshi ya MONUSCO, Jenerali Dos Santos Cruz katika [...]

10/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bila ushirikiano kutoka kwa serikali hatuwezi kufanya kazi ya haki za binadamu:UM

Kusikiliza / baraza la haki za binadamu

  Chombo kikubwa huru cha mfumo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo kimezitaka serikali kushirikiana nacho na kuruhusu mashirika ya haki za binadamu na watu binafsi kushirikiana na Umoja wa mataifa bila hofu ya kutishwa au ghasia. Wito huo kutoka kwa wataalamu maalumu 72 umekuja siku ya kimataifa ya haki za binadamu [...]

10/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Siku ya haki za binadamu, OPCW yakadhibiwa tuzo ya Nobel, ILO yalilia haki za wafanyakazi

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa OPCW Ahmet Üzümcü akikabidhiwa tuzo ya amani ya Nobel mjini Oslo

Katika kuadhimisha siku ya haki za binadamu duniani hii leo, mashirika mbali mbali ya Umoja wa Mataifa yameangazia ukiukwaji wa haki za binadamu katika sekta mbali mbali ikiwemo ile ya afya, ajira huku siku hii hii ya leo ikimulikwa wakati shirika la kimataifa la kupinga silaha za kemikali, OPCW,  ikipokea tuzo yake huko Oslo Norway. [...]

10/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO na washirika wazindua mpango mpya wa kuboresha afya ya akili

Kusikiliza / Wagonjwa wa akili katika kituo kimoja cha tiba huko India

Mpango mpya unaojumuisha taarifa mbalimbali kuanzia zile zinazohusu afya, haki za binadamu sera na watu wenye ulemavu umezunduliwa leo na kutoa mwanga mpya wa matumani duniani. Mpango huo ambao umezinduliwa ushirikiano wa pamoja baina ya MiNDbank,na shirika la afya ulimwenguni WHO unaweka viwango vinavyopaswa kufutwa na mataifa mbalimbali duniani. George Njogopa na maelezo kamili (RIPOTI [...]

10/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakati Mandela akipumzika kwa amani ni wakati wa kumuenzi kwa vitendo:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu, UM Ban Ki-moon na picha ya hayati Nelson MAndela(picha ya UN/MArio Salerno

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameungana na mamilioni ya watu wa Afrika ya Kusini, familia ya Marehemu Nelson Mandela, viongozi mbalimbali , watu mashuhuri na dunia kwa ujumla kutoa heshimazake za mwisho kwa jabali la Afrika na mtetezi wa haki duniani mzee Madiba, Nelson Mandela. Assumpta Massoi na taarifa kamili (MUSIC) Hivyo [...]

10/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Watu wanaokimbia ghasia Jamhuri ya Afrika ya Kati wanahitaji misaada ya dharura:IOM

Kusikiliza / Wakimbizi wa CAR

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linatoa huduma za dharura kwa wale walioathiriwa na mapigano kwenye Jamhuri ya Afrika ambapo mapigano Kati ya jamii yamevuruga nchi na kusababisha vifo vya watu 400 na wengine kuhama. Watu wengi wanalala nje kweneye maeneo ya mji wa Bangui. Inakadiriwa kuwa watu 60,000 waliolazimika kuhama makwao wanaishi kwenye misikitini [...]

10/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mahitaji ya misaada yazidi kuongezeka nchini Syria: UNHCR

Kusikiliza / Waliofurushwa makwao Syria

Tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2013 shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limewapelekea zaidi ya watu milioni tatu misaada wakiwemo wakimbizi wa ndani pamoja na wale wanaotaabika wanaohitaji usaidizi. Flora Nducha na taarifa kamili  (RIPOTI YA FLORA NDUCHA) Msaada wa UNHCR umewafikia wasyria wote kwenye majimbo manne huku takriban malori 250 [...]

10/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031