Nyumbani » 06/12/2013 Entries posted on “Disemba 6th, 2013”

Mandela Akumbukwa na watu mbali mbali duniani

Kusikiliza / nm3

  Mnamo Alhamisi Disemba 5 Nelson Mandela alifariki huko Afrika kusini akiwa na umri wa miaka 95. Kifo chake kimehuzunisha ulimwengu mzima kwani alikuwa  kiongozi  mashuhuri na mtetezi wa haki za bindamu ambaye alifahamika na kusifika kote ulimwenguni. Basi katika kumbuka Mzee Mandela, ungana na Joshua Mmali kwa makala ifuatayo Oktoba 1994. Rais wa kwanza [...]

06/12/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

UM wataka uchunguzi dhidi ya ukiukaji haki unaofanywa na wawindaji Ivory Coast:

Kusikiliza / Moja ya vikao vilivyoandaliwa na UNOCI kuelimisha wawindaji asili juu ya kuheshimu haki

Ripoti ya Umoja wa mataifa imetoa wito wa kufanyika uchunguzi dhidi ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliotekelezwa na wawindaji wa asili wajulikanao kama Dozos  kati ya mwezi Machi 2009 na Mei mwaka 2013 nchini Ivory Coast. Ripoti hiyo iliyotolewa leo na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNOCI kwa kushirikiana na ofisi [...]

06/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban na Nkurunziza wajadilia maandalizi ya uchaguzi wa Burundi wa 2015:

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, Paris

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza mjini Paris kandoni mwa mkutano wa Elysée unaohusu amani na usalama barani Afrika. Viongozi hao wawili wamejadili mengi miongoni mwa hayo ni hali nchini Somalia. Ban ameishukuru serikali yaBurundikwa mchango wake mkubwa wa mchakato wa amani nchiniSomalia. Pia wakagusia hali [...]

06/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ahudhuria mkutano wa amani Afrika, asema mizozo bado tatizo

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon akutana na Rais wa DRC Joseph Kabila Kabange

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye yuko mjini Paris Ufaransa kuhudhuria mkutano wa siku mbili kuhusu amani na usalama barani Afrika amesema kuendelea kwa mizozo barani humo ni moja ya mambo ya kutazamwa. Katibu Mkuu Ban amesema licha ya Umoja wa Mataifa kusaidia katika utatuzi wa migogoro lakini tishio la vikundi vyenye [...]

06/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mzee Nelson Mandela hakuwa mtu wa kujikuza: Naibu Mkuu UNAMA

Kusikiliza / Nicholas Haysom, Naibu Mkuu wa UNAMA ambaye aliwahi kuwa Mshauri Mkuu wa masuala ya sheria wa Mzee Mandela

Nicholas Haysom, raia wa Afrika Kusini ambaye alifanya kazi ya Mshauri Mkuu wa masuala ya Sheria kwa Mzee Nelson Mandela wakati wa kipindi chake chote cha Urais na hata baada ya kustaafu wadhifa huo, amesema Madiba hakuwa mtu wa kujikuza. Haysom ambaye kwa sasa ni Naibu Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchiniAfghanistan, [...]

06/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Rais Mstaafu wa Tanzania aungana na dunia kumuenzi Mzee Mandela

Kusikiliza / Mzee Mandela akitambulishwa na Mwl Nyerere kwenye uwanja wa Taifa jijini DSM wakati wa ziara nchini Tanzania

Madiba amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 na ulimwengu mzima umegubikwa na machozi! Kumbukumbu ya kile alichofanyia ulimwengu huu kuhakikisha maisha yanakuwa bora kwa wengi hususan huko Afrika Kusini na hata kugusa maisha ya wananchi wengine, hakitosahaulikaAbadan! Joshua Mmali katika ripoti hii fupi anaangazia kumbukumbu ya  Mzee Madiba!

06/12/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM aitaka Azerbaijan kuwalinda wanawake

Kusikiliza / Rashida Manjoo

  Mjumbe huru wa Umoja wa Mataifa Rashida Manjoo  leo ameitaka Azerbaijani kutekeleza kikamilifu sheria ya sasa na pia kuwachukuliwa hatua kali si wale tu waliohusika na vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake bali hata wale ambao walishindwa kuzuia vitendo hivyo. Amesmea kuwa mamlaka za dola zinapaswa kuhakiisha kwamba vitendo vyote vya unyanyasaji dhidi ya [...]

06/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kifo cha Mandela: Burundi yatangaza siku tatu za maombolezo

Kusikiliza / Mzee Mandela akilakiwa na aliyekuwa Rais wa Burundi Pierre Buyoya mjini Bujumbura mwaka 2003

Burundi imetangaza  siku tatu za maombolezo kufuatia kifo cha mzee Nelson Mandela. Mandela atakumbukwa katika nchi hiyo kutokana na jukumu  lake la kuwasuluhisha warundi baada ya mgogoro wa muda mrefu na kufikia makubaliano ya Arusha ambayo ni  msingi wa  taasisi za nchi hiyo na utengamano wa taifa. Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani KIBUGA ametuandalia [...]

06/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM yatoa ombi la dola milioni 13 kushughuliia mahitaji wa raia wa Ethiopia wanorejea nyumbani kutoka Saudi Arabia.

Kusikiliza / IOM yasaidia waEthipia kurudi nyumbani

Shirika la kimtaifa la uhamiaji IOM limetoa ombi la dola milioni 13.1 kuweza kushughulikia mahitaji ya karibu wahamiaji 120,000 raia wa Ethiopia  wanaorejea nyumbani  kutoka nchini Saudi Arabia huku idadi ya wahamiaji wanaorejea nyumbani ikizidi kuongezeka . Hadi jana Alhamisi zaidi ya wahamiaji 100,000 walikuwa wamepokelewa na serikali ya Ethiopia. Kati ya hao IOM ilitoa [...]

06/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sita kati ya watu kumi nchini Yemen watahitaji msaada:OCHA

Kusikiliza / Watu karibu milioni 15 wanahitaji msaada Yemen:OCHA

Watu sita kati ya watu kumi nchini Yemen wakiwa ni watu milioni 15 kati ya watu wote milioni 25 watahitaji misaada ya kibinadamju mwaka ujao kwa mujibu wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA. Jason Nyakundi na maelezo kamili.  (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) OCHA inasema kuwa makadirio hayo yanatokana na  wito [...]

06/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake na watoto walengwa wakati wa uhalifu CAR

Kusikiliza / Mwanaume huyu alia baada ya kunusurika kifo baadaya ya mashambulizi nchini CAR (picha ya UNHCR)

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameingia na wasiwasi kufuatia kuendelea kudororo kwa hali ya usalama Jamhuri ya Afrika ya Kati na kueleza kuwa hali hiyo inaweza kukwamisha juhudi wa kuwafikia zaidi ya watu milioni 2.6 ambao wanahitaji misaada. George Njogopa na taarifa kamili.  (TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA) Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto [...]

06/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kifo cha Mzee Mandela, bendera ya UM yapepea nusu mlingoti

Kusikiliza / Bendera ya UN yapeperushwa nusu mlingoti kwa ajili ya Mandela

Majonzi, huzuni vimeendelea kughubika ulimwengu kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela, aliyefahamika kutokana na ujasiri wake wa kupigania haki kwa maslahi ya wanaokandamizwa. Ndani ya Umoja wa Mataifa ambako misingi inayosimamiwa ya haki, amani, ulinzi na usalama Mzee Mandela aliipigania, saa Nne Asubuhi bendera za mataifa ya nchi wanachama kwenye makao makuu mjiniNew Yorkzilishushwa huku [...]

06/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC yasema Mandela hakutaka ukiukwaji wa haki

Kusikiliza / ICC

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC huko The Hague, imeungana na watu wa Afrika ya Kusini, bara la Afrika na jumuiya ya kimataifa kuombeleza kifo cha jabali wa Afrika, Mzee Nelson Mandela aliyekuwa sauti ya usawa na haki. ICC imesema ni wakati utawala wa Mandela mnamo Julai 17 mwaka 1998 nchi ya Afrika ya Kusini [...]

06/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mandela alifuata maadili kuliko kiongozi yeyote wa zama za sasa: Pillay

Kusikiliza / Hayati Nelson Mandela

Mzee Madiba , Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela aliyeaga dunia Alhamisi anatambulika kama kinara wa uhuru, usawa na haki za binadamu. Hayo yamesemwa na Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Navi Pillay aliyeongeza kuwa Mandela pengine ndiye kiongozi mfuata maadili kuliko mwingine yeyote katika kizazi hiki. Amesema [...]

06/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kenya wasema Mzee Mandela hakuna wa kulinganishwa naye

Kusikiliza / Mzee Mandela alipotembelea Kenya mara tu baada ya kutoka gerezani

Nchini Kenya Rais Uhuru Kenyatta na wananchi wake wametoa salamu kwa Taifa la Afrika Kusini, familia na wananchi kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela, na hiyo ni katika salamu za rambirambi na maoni yao kama anavyoripoti mwandishi wetu wa Nairobi, Jason Nyakundi. (Ripoti ya Jason) Kifo cha Mzee Mandela kimegusa wengi siyo tu Afrika Kusini [...]

06/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031