Nyumbani » 05/12/2013 Entries posted on “Disemba 5th, 2013”

Mandela alitetea maadili ya haki na maridhiano: Rais Baraza la usalama

Kusikiliza / Baraza la Usalama wakati wa dakika moja ya kumkumbuka Mandela

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo walilazimika kusitisha kikao chao cha kupokea ripoti kuhusu mahakama za za uhalifu wa kimbariRwanda, ICTR na mahakama ya uhalifu ya taifa la zamani laYugoslavia, ICTY ili kuugana na ulimwengu kwenye maombolezo ya kifo cha Mzee Nelson Mandela. Wajumbe walisimama kwa dakika moja kumkumbuka Mzee na [...]

05/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kifo cha Mandela: Baraza Kuu la UM lasema ni masikitiko makubwa

Kusikiliza / Mzee Nelson Mandela alipohutubia Baraza Kuu la UM

Salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mzee Mandela zimeendelea kutolewa na za hivi punde zinatoka kwa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa John William Ashe ambaye amemwelezea Mzee Mandela kuwa ni alama ya amani duniani na gwiji wa maadili miongoni mwa viongozi wa zama za sasa. Bwana Ashe amesema wakati wa uhai wake [...]

05/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lasikiliza ripoti za maandalizi ya kuhitimisha majukumu ya ICTR na ICTY

Kusikiliza / Wajumbe wa Baraza la Usalama wakinyoosha mkono kupiga kura

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo mchana limesikiliza ripoti za kila baada ya miezi sita za mahakama za uhalifu wa kimbari Rwanda, ICTR na mahakama ya uhalifu ya taifa la zamani la Yugoslavia, ICTY. Akilihutubia Baraza hilo, Rais wa Mahakama ya ICTR, Jaji Vagn Joensen amesema baada ya takriban miongo miwili ya uendeshaji [...]

05/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Nelson Mandela afariki dunia: Ban atuma rambirambi

Kusikiliza / Nelson Mandela

Nelson Mandela, Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini amefariki dunia. Alikuwa na umri wa miaka 95.  Kifo cha Mandela kimetangazwa na Rais Jacob Zuma kupitia televisheni ya nchi hiyo. Kufuatia kifo hicho Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza na waandishi wa habari mjini New York..  (Sauti ya Ban Ki-Moon) "Nimesikitishwa sana na [...]

05/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Azimio kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati limekuja wakati muafaka: Ban

Kusikiliza / Maisha ya wananchi wa CAR ni ya kuhamahama kutokana na mizozo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha kitendo cha Baraza la Usalama kupitisha azimio namba 2127 linaloidhinisha kupelekwa kwa vikosi vya Umoja wa Afrika na vile vya Ufaransa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Katika taarifa, Bwana Ban amekaririwa akisema uamuzi huo umekuja wakati muafaka na kwamba unatuma ujumbe wa azma ya jamii [...]

05/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban alaani vikali shambulizi la bomu Yemen

Kusikiliza / Ramana ya Yemen

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amelaani vikali shambulio la kigaidi lililotekelezwa leo dhidi ya Wizara ya Ulinzi ya Yemen na ambalo limeripotiwa kuwaua watu 20 na kuwajeruhi wengine wengi. Bwana Ban ametoa wito kwa wote wanaohusika kushirikiana kikamilifu na uchunguzi ulotangazwa kufanyika na Rais Abed Rabbo Mansour Hadi, wenye nia ya kuwawajisbisha [...]

05/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Malala Yousafzai ashinda tuzo ya heshima ya UM

Kusikiliza / Malala Yousafzai

Mtoto Malala Yousafzai ambaye ni mwanaharakati wa haki ya elimu kwa mtoto wa Kike kutoka Pakistani, ni miongoni mwa washindi Sita wa tuzo ya heshima ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka huu wa 2013. Kamati ya uteuzi imesema Malala na washindi wengine wamepatiwa tuzo hiyo kutokana na mchango wao wa kipekee [...]

05/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Raia wa Guatemala anayejitolea Tanzania aeleza jinsi anavyoithamini kazi hiyo

Kusikiliza / Nataly Monila, raia wa Guatemala anayefanya kazi ya kujitolea huko mkoani Tanga nchini Tanzania.

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kujitolea inaelezwa kuwa umuhimu wa siku hii ni katika kukuza amani na maendeleo duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema  mchango wa wanaojitolea unatambulika. Miongoni mwa wanaojitolea ni Nataly Monila raia wa Guatemala anayefanya kazi za kufundisha mkoani Tanga nchini Tanzania na katika mahojiano na [...]

05/12/2013 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lapitisha azimio la kuruhusu vikosi vya kurejesha utulivu CAR

Kusikiliza / Wajumbe wa Baraza la Usalama wakipiga kura

Wakati hali tete ikiwa imetanda kwenye mji mkuu wa Bangui katika Jamhuri ya Aftrika ya Kati kufuatia shambulizi lililosababisha vifo vya raia, Baraza la Usalama limechukuwa hatua mathubuti kurejesha utulivu nchini humo. Joshua Mmali na taarifa kamili. (TAARIFA YA JOSHUA) Katika azimio lililoungwa mkono na kupitishwa kwa kauli moja, Baraza la Usalama la Umoja wa [...]

05/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

AMISOM yaratibu warsha kuhusu idara za mahakama Somalia

Kusikiliza / somali women

Ujumbe wa muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM kwa ushirikiano na serikali yaSomalia na mashirika ya kiraia Alhamisi wamekamilisha warsha yenye lengo la kuboresha idara za sheria nchini humo ili kuwezesha kuhudumia masuala yanayohusina na dhuluma za kijinsia. Warsha hiyo ililenga kuhakikisha kuwa haki za wanawake zinaheshimiwa, ilihudhuriwa na wawakilishi wa serikali ya Somalia wanaofanya [...]

05/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

FAO yaonya kuhusu hali ya chakula Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Wananchi wa Jamhuri ya Afrika  ya Kati wakipatiwa mgao wa chakula kutoka WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la  chakula na kilimo FAO limesema Uzalishaji wa mazao na nafaka duniani unatazamia kufikia kiwango cha juu ambacho ni karibu tani milioni 2,500 ikiwemo mpunga . FAO inaonya kuwa zaidi ya watu milioni 1.3 katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wanahitaji msaada wa chakula kutokana na machafuko yanayoendelea. George Njogopa [...]

05/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya amani Kivu Kaskazini yaridhisha lakini hatua zaidi zahitajika: Ladsous

Kusikiliza / Herves Ladsous wakati wa uzinduzi wa ndege zisizo na rubani, drones kwa ajili ya kuimarisha amani DRC

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa Herves Ladsous ametembelea jimbo la Kivu Kaskazini huko DR Congo na kusema kuwa hali imekuwa shwari kwenye eneo la Pinga lakini bado kuna hatua madhubuti za kuchukua kuimarisha usalama. Radio washirika Okapi imemkariri Bwana Ladsous akisema hayo katika siku ya tatu ya ziara yake [...]

05/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji 100,000 raia wa Ehiopia warejea nyumbani kutoka nchini Saudi Arabia

Kusikiliza / IOM yasaidia kurejesha nyumbani waEthipia walioko Saudia

Idadi ya wahamiaji raia wa Ethiopia wanaorejea nyumbani kutoka nchini Saudi Arabia imepita watu 100,000 kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Jason Nyakundi na maelezo kamili. (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) IOM inasema kuwa shughuli ya kurejea nyumbani kwa wahamiaji hao ina gharama kubwa na inatoa ombi la dola milioni 13 za kuwasaidia [...]

05/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM Somalia alaani shambulio la Bossaso

Kusikiliza / Mwakilishi wa UM, Somalia Nicholas kay

Mwakilishi maalumu wa UM nchini Somalia Nicholas Kay, amelaani vikali shambulio la kikatili dhidi ya majeshi ya serikali huko Puntland . Katika shambulio hilo la Jumatano alfajiri mshambuliaji wa kujitoa mhanga akiwa na mabomu kwenye gari alilenga vikosi vya serikali mjini Bossaso. Kwa mujibu wa duru za habari mjini humo watu kadhaa wameuawa na wengine [...]

05/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mchango wa wanaojitolea duniani unatambulika:Ban

Kusikiliza / Nembo

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kujitolea , mchango wa wale wote wanaofanya hivyo kwa ajili ya amni na maendeleo ya kimataifa mchango wao unatambulika. Hayo yamesemwa na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwenye ujumbe maalumu wa kuadhimish siku hii. Ameongeza kuwa leo hii watu zaidi ya biioni 1.2 duniani ambao ni [...]

05/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031