Nyumbani » 03/12/2013 Entries posted on “Disemba 3rd, 2013”

Ban azungumzia umuhimu wa wanawawake, asasi za kiraia katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi .

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumzia umuhimu wa asasi za kiraia , viongozi wa kijamii na wanawake katika kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Katika mkutano na waziri wa mazingira wa Peru Manuel Pulgar-Vidal, katibu mkuu ambaye anahitimisha ziara yake nchini humo amesema anajivunia namna wanawake na asasi za kiraia [...]

03/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tunajali haki za walemavu: Tanzania

Kusikiliza / Ulemavu

Haki na ustawi wa watu wenye ulemavu ni kipaumbele cha serikali ya Tanzania, amesema rais wa nchi hiyo Jakaya Kikwete wakati akihutubia taifa hilo kwenye maadhimisho ya siku hiyo yaliyofanyika kitaifa mjini Dar es salaam. Wakati rais Kikwete akisisitiza kujali maslahi ya kundi hilo, walemavu wenyewe wanadai bado hawapati msaada kama wanavyotarajia. Mwandishi wa radio [...]

03/12/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Tamasha la uelewa wa Ukimwi lafanyika Tanga, Tanzania

Kusikiliza / maadhimisho ya siku ya ukimwi

  Wakati dunia ikiadhimisha siku ya ukimwi duniani mwishoni mwa wiki, maadhimisho haya yameleta mwanga bora mkoani Tanga nchini Tanzania ambapo tamasha kubwa limefanyika katika wailaya ya Pangani ili kukuza uelewa wa wananchi. Muhamedi Hamie kutoka radio washirika Pangani Fm, Tanga Tanzania, amefika katika tamasha hilo na kuandaa makala ifuatayo

03/12/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wasikitishwa na ghasia Jahmhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Mtoto katika eneo moja lililoathirika kwa mapigano

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na ujenzi wa amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, BINUCA, imeelezea masikitiko yake kufuatia matukio ya ghasia katika eneo la Boali, yapata kilomita 95 kutoka mji mkuu wa Bangui, ambapo raia wameuawa na wengine kujeruhiwa. Watu wapatao 12 wameuawa, huku wengine 30 wakijeruhiwa, wakiwemo watoto kutokana na ghasia [...]

03/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ripoti mpya yatoa suluhu kupunguza mwanya wa chakula duniani

Kusikiliza / Kilimo

Hatua madhubuti zinahitajika ili kuboresha uzalishaji wa chakula ili kundoa mwanya wa asilimia 70 uliopo duniani. Utafiti mpya uliofanywa umeangazia baadhi ya suluhu  katika kukabiliana na mahitaji ya chakula yanayozidi kuongezeka duniani. Tathmini hiyo inaeleza kuwa ulimwengu utahitaji asilimia 70 zaidi ya chakula kuweza kulisha watu bilioni 9.6 ifikapo mwaka 2050. Kwenye miongo kadha inayokuja [...]

03/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Usambazaji misaada Syria watia moyo, hatua zaidi zahitajika: OCHA

Kusikiliza / Mkuu wa OCHA Valerie Amos

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na usaidizi wa binadamu, OCHA, Bi. Valerie Amos amelieleza baraza la usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kuwepo kwa matumaini  ya kupanuka kwa wigo wa usambazaji wa misaada ya kibinadamu nchiniSyriakufuatia taarifa ya Rais wa barazahiloya tarehe Pili Oktoba mwaka huu. Taarifa hiyo kuhusu hali ya [...]

03/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko ya sheria ya jumuiya za kijamii Kenya yatakuwa na athari:UM

Kusikiliza / Nembo ya UN

Kundi la wawakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu  leo wameitaka serikali ya Kenya kuipinga sheria itakayoweka vikwazo vigumu kwa jumuiya za kijamii. Mswada huo ni ushahidi dhahiri kwa kuongezeka kwa mwenendo wa mataifa ya Afrika na kwingineko ambako serikali zinajaribu kuchukua udhibiti zaidi wa makundi huru kwa kutumia kile wanachi walikiita [...]

03/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ondoa vizuizi, fungua milango, jumuisha walemavu katika maendeleo: Ban

Kusikiliza / Watu wenye ulemavu waingia shule ya Romania inayotoa mafunzo kwao, (picha ya benki ya dunia)

Leo ni Siku ya Kimataifa ya watu wenye ulemavu, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametoa wito viondolewe vikwazo ili kuhakikisha kuwa takriban watu bilioni moja wanaoishi na ulemavu kote duniani wanajumuishwa katika jamii kikamilifu. Joshua Mmali ana taarifa kamili Ujumbe wa Katibu Mkuu ulopambwa kwa video maalum, umeenda sambamba na kauli [...]

03/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kila mtu atanufaika tukijumuisha walemavu kwenye ajira: ILO

Kusikiliza / ILO yapendekeza watu wenye ulemavu wajumuishwa kazini

Hali ya wanawake na wanaume walemavu kwenye soko la ajira linatia hofu na mashaka makubwa kwani wana fursa ndogo zaidi ya kuajiriwa kuliko wasio walemavu na hata wakiajiriwa wengi wao huwekwa katika sekta ambazo malipo yake ni haba. Amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kazi duniani, ILO Guy Rider katika kuadhimisha siku ya walemavu hii [...]

03/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yalazimika kupunguza huduma zake nchini DRC kutokana na ukosefu wa fedha

Kusikiliza / Usambazaji wa chakula DRC

 Shirika la mpango wa chakula duniani WFP  limesema kuwa litalazimika kupunguza baadhi ya huduma zake kuanzia mwezi huu kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi yaCongohatua ambayo itawaacha maelfu ya watu bila msaada wowote. Flora Nducha na taarifa kamili. (RIPOTI YA FLORA NDUCHA) Ilikuendelea na oparesheni zake kwa kipindi cha miezi sita inayokuja WFP inahitajia dola milioni 75 [...]

03/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto nchini Syria kuathiriwa na baridi kali:UNICEF

Kusikiliza / Watoto kuathirika na baridi kali

Wakati baraza la usalama la Umoja wa Mataifa likifanya mashauriano kuhusu mustakabali wa amani ya Syria, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema kiasi cha watoto milioni 5.5 wa Syria wanatazamia kutumbukia kwenye adha nyingine wakati kipindi cha msimu wa baridi kitapoanza hatua ambayo inatazamia kuwaweka kwenye hatari kubwa juu ya afya [...]

03/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu zaidi ya 15,000 wanahitaji misaada ya dharura Niger:OCHA

Kusikiliza / Mafuriko Niger

Zaidi ya watu 15,000 wapo katika hali mbaya Kusin Mashariki mwaNigerna kwamba misaada ya dharura inahitajika ili kunusuru maishayaokufuatia mafuriko makubwa yaliyosababishwa na kubasuka kwa kingo za  mto Komadougou . Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya usamaria mwema OCHA limesema kuwa mafuriko hayo yalianza kujitokeza katika kipindi cha miezi michache iliyopita na [...]

03/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wagonjwa wengine watatu waliokumbwa na virusi (MERS-CoV) wagundulika Abu Dhabi

Kusikiliza / Ngamia mnyama anayesemekana kueneza kirusi hicho

Shirika la afya ulimwenguni WHO limearifiwa juu ya kugundulika kwa wagonjwa wengine watatu wenye matatizo ya virusi vya (MERS-CoV) katika eneo la Mashariki baada ya uchunguzi wa kimaabara kukamilika. Wagonjwa hao watatu ni kutoka familia moja iliyoko Abu Dhabi ambao ni mama mwenye umri wa miaka 32, baba mwenye wa miaka 38 na mtoto wa [...]

03/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM na Ethiopia washirikiana kusaidia wahamiaji wanaorejea nyumbani:

Kusikiliza / Nembo ya IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na serikali ya Ethiopia wanashirikiana kusaidia wimbi kubwa la wahamiaji wanaorejea nyumbani Ethiopia kutoka ufalme wa Saudi Arabia. Takribani wahamiaji 7,000 wanawasili kila siku mjiniAddis Ababawakitokea Saudia. Wahamiaji 75,000 wamesharejea tangu kuanza kwa operesheni hiyo tarehe 13 Novemba huku 47,479 wakiwa wanaume, 25,000 wanawake na watoto ni 3,391. Wahamiaji [...]

03/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031