Nyumbani » 02/12/2013 Entries posted on “Disemba 2nd, 2013”

Mkuu wa UNSOM azungumzia kuondolewa kwa Waziri Mkuu Somalia

Kusikiliza / Abdi Farah Shirdon

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay amezungumzia vile ambavyo wabunge wa bunge la nchi hiyo na spika wake walivyoendesha kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu wa nchi hiyo Abdi Farah Shirdon. Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM, Bwana Kay pamoja [...]

02/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Burundi yakabiliwa na changamoto ikijiandaa na uchaguzi wa 2015:

Kusikiliza / PARFAIT ONANGA-ANYANGA

Mchakato wa kuelekea uchuguzi mkuu wa Burundi hapo 2015 uliopitishwa mapema mwaka huu umetathiminiwa wiki hii na vyama vya siasa vya Burundi na wadau wengine kwenye mkutano wa siku tatu ulioandaliwa na serikali yaBurundi na ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo BNUB. Mkutano huo ulioanza Novemba 27 na kukamilika Novemba 29 umetathimini utekelezaji wa [...]

02/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mratibu wa UM Afghanistan asikitishwa na vifo vya wafanyakazi wa misaada

Kusikiliza / Ramana ya Afghanistan

Mark Bowden, mratibu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya Afghanistan ameelezea huzuni yake kufuatia vifo vya wafanyakazi 9 wa misaada wa Afghanistan katika mashambulio mawili tofauti siku za karibuni. Amesema hadi kufikia sasa mwaka huu pekee Umoja wa Mataifa umerekodi visa 237 dhidi ya wafanyakazi wa misaada, majengo na vifaa vya wafanyakazi hao. Katika [...]

02/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Makubaliano ya Bali yaruhusu sera kabambe kuhusu uhakika wa chakula: Mtaalamu UM

Kusikiliza / Kikao cha WTO, Bali, Indonesia

Wakati macho na masikio yameelekezwa huko Bali, Indonesia ambako tarehe Tatu mwezi huu kunaanza mkutano wa siku tatu wa mawaziri wa nchi wanachama wa shirika la biashara duniani, WTO,  wito umetolewa kwa nchi zinazoendelea kupatiwa uhuru wa kutumia chakula cha akiba kwa ajili ya hakikisho la usalama wa chakula bila ya woga ya vitisho vya [...]

02/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Huduma za kibinadamu zatangulizwa wakati Ufilipino ikijikwamua kutoka kimbunga Haiyan: UM

Kusikiliza / Harakati za kujikwamua baada ya kimbunga Haiyan Ufilipino

Kufikisha huduma za kibinadamu kwa manusura wa kimbunga Haiyan bado ni suala la kipaumbele kwa mfumo wa Umoja wa Mataifa na wadau wake, amesema Bwana Haoliang Xu, Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya Mpango wa Maendeleo katika Umoja wa Mataifa, UNDP kwenye eneo la Asia na Pasifiki, ambaye pia ni Msimamizi wa Ofisi ya kikanda ya [...]

02/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNIDO ina dhima muhimu kuelekea uzalishaji viwandani ulio rafiki kwa mazingira: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon akiwa Peru

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amefungua mkutano Mkuu wa 15 wa Shirika la maendeleo ya viwanda la Umoja wa Mataifa , UNIDO huko Lima, Peru akiangazia umuhimu wa taasisi hiyo katika kuwezesha dunia kufikia maendeleo endelevu hata baada ya mwaka 2015. Bwana Ban amesema sasa kuna kasi ya kutimiza malengo ya maendeleo [...]

02/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Upatikanaji wa maji ni habari njema kwa jamii ya wafugaji Tanzania

Kusikiliza / Wafugaji Tanzania

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wahisani imekuwa ikijitahidi kutekeleza malengo ya maendeleo ya milenia katika maeneo mbalimbali ikiwamo kuboresha huduma ya maji vijijini na mijini. Makala ifuatayo inaangazia miongoni mwa eneo kame kabisa Kaskazini mwa nchi hiyo ambapo kwa asilimia kubwa jamii ya wafugaji wa kimasaia ndiyo inaishi huko. Ungana na Joseph Msami.

02/12/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Utumwa nchini Ghana bado unatesa watoto: Mtaalamu

Kusikiliza / Watoto nchini Ghana

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu vitendo vya utumwa vinavyofanyika sasa duniani, Gulnara Shahinian ameitaka serikali ya Ghana kuimarisha hatua zake za kukabiliana na vitendo vya utumwa nchini humo. Bi. Shahinian amesema hayo leo ambapo dunia inaadhimisha siku ya kutokomeza aina zote za utumwa akieleza bayana kuwa nchiniGhana, utumwa bado uko dhahiri hata kwa [...]

02/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa haki za binadamu azuru Sri Lanka kutathimini hali ya wakimbizi wa ndani

Kusikiliza / Kambi za wakimbizi

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu Chaloka Beyani ameanza leo ziara ya siku tano nchini Sri Lankakutathimini hali jumla ya wakimbizi wa ndani nchini humo. Amesema nia ni kwenda kukusanya taarifa kutoka pande zote zikiwemo za wakimbizi wa ndani na jamii zilizoathirika  hasa mjiniColombo,Jaffnana Mullaitivu. Bwana Beyani pia ataangazia changamoto na fursa [...]

02/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uongozi wa Syria wahusika na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu:Pillay akinukuu ripoti

Kusikiliza / Navi Pillay

Uongozi wa ngazi ya juu wa Syria unahusika na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliotekelezwa  wakati wa machafuko yanayoendelea nchini humo amesema mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay akinukuu ripoti ya uchunguzi. Assumpta Massoi na ripoti kamili (RIPOTI YA ASSUMPTA MASSOI) Akizungumza mjini Geneva Bi Pillay amesema ripoti za [...]

02/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres ataka maisha ya baadaye ya watoto wa Syria kutiliwa maanani

Kusikiliza / Mkuu wa UNHCR kuhusu hali ya watoto Syria

Kamishina mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, Antonio Guterres amelipongeza taifa la Lebanon kutokana na utu wake lilipojitolea kuwapa hifadhi zaidi ya watu 800,000 ambapo pia ameyataka mataifa wahisani kutoa misaada ya kifedha . Mkuu huyo wa UNHCR ambaye tayari ameutembelea mji wa Arsal nchini Lebanon mji ulio bonde la [...]

02/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Utumwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu: Ashe

Kusikiliza / Utumwa

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya kutokomeza utumwa, rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, John William Ashe, amesema utumwa wa nyakati za sasa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za kimsingi za binadamu. Joshua Mmali na taarifa kamili. (TAARIFA YA JOSHUA) Katika ujumbe wake kuadhimisha siku hii, Bwana Ashe amesema utumwa huenda umekuwa, [...]

02/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bila hatua madhubuti, tembo wa Afrika kutoweka muongo ujao

Kusikiliza / Uhai wa tembo Afrika uko mashakani

Nchini Botswana kunafanyika mkutano wa kubaini mustakhbali wa tembo wa Afrika ambao maisha yao yako mashakani kila uchao kutokana an vitendo vya kijangili. Mkutano huo uliotishwa na serikali ya Botswana kwa ushirika na shirika la kimataifa la uhifadhi wa maliasili, unafanyika wakati takwimu mpya zikisema kuwa bila hatua madhubiti, tembo hao baada muongo ujao watabakia [...]

02/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kenya tunga sera zinazochochea ongezeko la ajira:ILO

Kusikiliza / Mfanya biashara (picha ya AFP)

Shirika la kazi duniani , ILO limefanya utafiti kuhusiana na masuala ya ajira nchini Kenya na kubaini kuwa nchi hiyo yahitajika kuridhia mkakati wa kitaifa wa ajira utakaotoa fursa sawia za ajira kwa makundi yote ikiwemo vijana. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace Kaneiya) Utafiti huo wa ILO unaonyesha kuwa licha ya kiwango [...]

02/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majeraha ya uti wa mgongo ni mabaya lakini yanazuilika: WHO

Kusikiliza / Majeraha ya uti wa mgongo

Takribani watu Laki Tano kila mwaka duniani kote hukumbwa na magonjwa yatokanayo na majeraha kwenye uti wa mgongo ambapo wengi wao hulazimika kuishi na maumivu hayo katika maishayaoyote kutokana na ukosefu wa tiba sahihi. Hiyo ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani, wHO katika kuelekea siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu tarehe tatu [...]

02/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031