Zaidi ya visa 4,000 vya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana vyaripotiwa Afghanistan:

Kusikiliza /

Wanawake , Afghanistan picha ya UNAMA

Zaidi ya visa 4000 vya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana vimeripotiwa katika wizara ya wanawake ya Afghanistan kutoka majimbo 33 kwa mwaka 2010-2012 umesema mpango wa Umoja wa mataifa nchini humo UNAMA.

UNAMA inasema hatua za kutokomeza vitendo hivyo vya kikatili, vitisho na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kutawawezesha kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kisiasa na maendeleo ya kiuchumi na hiyo itachangia katika kuboresha maisha ya Waafghanstan wote.

Hata hivyo UNAMA inasema katika miezi ya karibuni Afghanistan imeshuhudia visa vingi vya ukatili ukiwemo utekaji na mauaji ya kulenga vinavyofanywa na wapinga serikali dhidi ya maafisa wa serikali wanawake na viongozi wengine. Kwa mujibu wa Mkuu wa UNAMA  Ján Kubiš, mashambulio hayo lazima yakome kwani yanawavunja moyo wanawake na wasichana kuingia katika masuala ya kijamii na kisiasa wakihofia maisha yao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031