Yemen yakiuka mkataba unaopiga marafuku silaha za ardhini

Kusikiliza /

Utafiti wa silaha ardhini

Yemen imekiri kuwa imekwenda kinyume na mkataba wa kimataifa unaopiga marafuku matumizi, kuhifadhi na kuzalisha kwa silaha za ardhini.

Kampeni ya kimataifa inayopiga marafuku silaha za ardhini imesema kuwa iliitaka serikali ya Yemen kuondosha maelfu ya silaha mwaka 2011 katika baadhi ya sehemu mbili. Kujitokeza kwa machafuko ya kiraia katika miaka ya hivi karibuni ni sehemu iliyochochewa na silaha hizo.

Shirika hilo la kimataifa limesema kuwa limepata ripoti zinazoonyesha kuwa silaha za ardhini zimetumika nchini humo katika miaka ya hivi karibuni jambo ambalo ni kwenda kinyume na mkataba wa kimataifa.

Ripoti hiyo inasema pia kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya silaha hizo kutoka kwa makundi ya watu mbalimbali ikiwemo makundi ya waasi. Mark Hiznay ndiye aliyehariri ripoti hiyo.

 

(SAUTI YA MARK HIZNAY)

"Katika mwaka 2002, Yemen ilitangaza kuwa inateketeza kabisa maghala ya silaha hizi na ikahaidi pia kuteketeza kiwango kingine cha silaha kilichogundulika mwaka 2007. Kwa hivyo kwa kuangalia mambo tangu mwaka 1999 Yemen ilikuwa haipaswi kutumia silaha hizi na haikupaswa kuwanazo kabisa.Tunamategemeo ya kupata ufafanuzi zaidi kutoka kwa serikali wiki ijayo na pia tunategemea kupata maoni mazito kutoka kwa nchi zilizosaini mkataba huu.”

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031