WHO yaendelea kuratibu misaada ya madawa Ufilipino:

Kusikiliza /

Kituo cha muda Ufilipino

Ikiwa ni zaidi ya siku kumi tangu kuzuka kwa kimbunga Haiyan nchini Ufilipino, shirika la afya duniani WHO linaendelea kuleta wataalamu wa kitabibu kutoka sehemu mbalimbali wanaokwenda Ufilipino .

Hivi sasa kwa mujibu wa shirika hilo wanajikita zaidi kwa majeruhi na wale walioathirika kisaikolojia na kimbunga hicho huku wakitilia maanani mahitaji ya muda mrefu ya kiafya ya manusura hao.Kwa sasa kuna timu ya wataalamu wa afya 22 wanaotoa msaada katika majimbo matatu na kila kimoja walikwa na mtaalamu kutoka Ufilipino pia.

Timu zingine 12 za wataalamu ama wako njiani au wanasubiri kkwenda Ufilipino na kuna timu 31 za kitaifa za Ufilipino ambazo zinatoa msaada katika maeneo yote yaliyoathirika nchini humo. Wataalamu 17 kati ya 22 wanashughulika na wagonjwa wa nje na huduma za dharura, watano wamejikita katika upasuaji ikiwa ni pamoja na kuzalisha kwa wanaohitaji huduma hiyo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031