WFP inaendelea kuongeza misaada CAR:

Kusikiliza /

Chakula

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linaendelea kuongeza operesheni za kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati licha ya hali kuzidi kuwa mbaya.  Shirika hilo limeshasambaza msaada wa chakula kwa maelfu ya watu mjini Basonga lakini limesema watu takribani milioni 2.9 wanahitaji msaada wa kibinadamu nchini humo.

Hivi karibuni tani 358 za chakula mchanganyiko zimegawanywa kwa wakimbizi wa ndani 29,000 na WFP ina mpango wa kugawa chakula kwa wapya 8000 waliotawanya na kukimbia mapigano mjini Basonga, na nje ya mji mkuuBanguiwatu milioni 1.3 wana matatizo ya chakula. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS

"Watu waliopoteza makazi wako hatarini zaidi, wamekimbia ghasia na sasa wamajificha vichakani na misituni, na hivyo ni vigumu kuwahudumia. Ndio maana WFP hivi sasa inafikiria kufungua tena ofisi zake huko Bombari, Kaga Bandoro ili kuendeleza kazi ya kusambaza misaada inayofanywa na timu zinazotembelea wananchi ambazo zinatuwezesha kuwahudumia wananchi kwenye maeneo yasiyo salama huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.”

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930