Wataalam wa UM kuchunguza hali ya watu wenye asili ya Afrika Brazil

Kusikiliza /

Watu wenye asili ya Afrika Brazil

Kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye asili ya Afrika litafanya ziara ya siku kumi nchini Brazil, kuanzia Disema 3 hadi 13 2013, ili kuchunguza masuala kadhaa yanayohusu haki za binadamu za watu wenye asili ya Afrika nchini humo.

Mmoja wa wataalamu hao, Mireille Fanon-Mendes-France amesema kuwa Brazil imepiga hatua nyingi katika kuendeleza usawa katika miaka ya hivi karibuni, lakini bado inakabiliwa na changamoto zinazohusiana na athari za utumwa, biashara ya utumwa na ukoloni, kama nchi nyingi za Amerika ya Kusini.

Ziara hiyo inatarajiwa kutoa nafasi ya kukagua jinsi Brazil inavyokabiliana na changamoto hizo, na kuisaidia serikali kutimiza wajibu wake kuhusu haki za watu wenye asili ya Afrika.  Pia wataitumia fursa hiyo kutathmini hatua zilizopigwa katika kutekeleza mapendekezo yalofanywa na mtaalam maalum wa kupinga ubaguzi wa rangi alipozuru Brazil mnamo mwaka 2005.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2016
T N T K J M P
« apr    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031