Wakimbizi zaidi wa Syria wakimbilia Lebanon

Kusikiliza /

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa zaidi ya familia 500 za Syria zimelazimika kuvuka mpaka siku ya jumatano usiku na kukimbilia eneo la Aarsal kutokana na kuenea kwa mapigano hadi katika maeneo ya Nabek na Yabroad. Shirika hilo linasema kuwa zaidi ya watu 10,000 wamepatiwa msaada wa chakula. Idadi ya wakimbizi walioandikishwa tangu Novemba 16 mwaka huu imefikia familia 3000 na juhudi za kuwasambazia chakula bado zinaendelea. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(Sauti ya Byrs)

"Wanapatiwa chakula mara moja, hakuna kusubiri hata kidogo na tunafanya kazi kwa karibu na UNHCR ili wakimbizi hao wapatiwe kile wanachohitaji. Halafu tunawapatia kadi ya kielektroniki ya kununua mahitaji na hii ni njia bora zaidi kwa sababu hakuna haja ya kwenda eneo la mgao wa chakula, kwa hiyo hakuna kusafirisha na wanaweza kutumia kununua kile wanachohitaji na familia zinafurahia sana mfumo huo."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930