Viwango vya gesi chavuzi angani vyavunja rekodi: WMO

Kusikiliza /

Gesi chafuzi

Viwango vya gesi zinazochafua mazingira angani vilifikia rekodi mpya mwaka 2012 huku vikizidi kupanda hali ambayo imesababisha kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya hali ya hewa na kuibadilisha sayari ya dunia kwa maelfu ya miaka inayokuja. Alice Kariuki anaripoti.

(Taarifa ya Alice)

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO kupitia kwa makala yake ya kila mwaka kuhusu gesi zinazochafua mazingira kati ya mwaka 1990 na 2012 inaonyesha kuwa kulikuwa na ongezeko la joto duniani kwa asilimia 32 kutokana na kuwepo kwa gesi zinazochafua mazingira angani. Mathalani hewa ya Ukaa ilichangia asilimia 80 kwa ongezeko hili.

Mkurugenzi Mkuu wa WMO Michel Jarraud amesema ongezeko hilo linazidisha mabadiliko ya tabianchi, hali ya hewa inakuwa si ya kawaida, barafu zinayeyuka, na hata viwango vya maji ya bahari vinaongezeka. Amesema kudhibiti ongezeko hilo kwahitaji upunguzaji endelevu wa utoaji wa gesi chafuzi.

(Sauti ya Michel)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031