UNHCR yawapatia mafunzo wakimbizi wa DR Congo nchini Uganda

Kusikiliza /

Wakimbizi wa DRC nchini Uganda

Huko nchini Uganda, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeanza kuwapatia wakimbizi wapya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC walioko kambi ya kambi ya Kyangwali mafunzo kuhusu haki zao ikiwemo ile ya ulinzi wa kimataifa pamoja na sheria. Hatua hiyo inakuja baada ya shirika hilo kubaini kuwa wakimbizi hao hawafahamu lolote kuhusu haki zao wakiwa ukimbizini kama anavyoripoti John Kibego wa Radio washirika ya Spice FM kutoka Uganda.

(Taarifa ya Kibego)

Katika warsha hizo wanaonywa wasijihusishe vyovyote na siasa ya Uganda, kutii sheria za nchi na pya wanajulishwa ni nani anayehusika na nini katika kuwahudimia.

Coliin Otee, afisa wa kutetea wakimbizi kwenye ofisi ya UNHCR ya Hoima anaeleza kuhusu warsha hizo.

(Sauti ya Otee)

"Tumekuwa na mkutano wa viongozi wa wakimbizi kuhusu ulinzi wa kimataifa.

Pya kuwajulisha jukumu la UNHCR, serikali ya Uganda, ma majukumu yao wenyewe.

Kwa upamde wa wajibu wao, wanatarjiwa kutii sheria za nchi walimokimbilia na tunasisitiza kwa kuwambizi wasijihushishe na siasa"

Polisi wa hapa mjini Hoima wamekuwa wakisema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya wakimbizi kutojua sheria za Uganda, na hata wakifungua mashitaka baada ya kukoseana, hawayafuatilii.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29