Msimu wa safari za mashua huko pwani ya Bengali zatia hofu UNHCR

Kusikiliza /

Mashua hizi za uvuvi hutumika kwa safari

Katika siku za karibuni shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limepokea taarifa za kutia hofu kwamba watu zaidi wanaondoka kwa kusafirishwa katika boti haramu kwenye Pwani ya Bengali, hali ambayo inaashiria kuanza kwa msimu wa kila mwaka wa safari za meli wakati ambao maelfu ya watu kutoka jimbo la Rakhine huko Myanmar wanahatarisha na kupoteza maisha wakijaribu kusafiri kwa boti kwenda kutafuta usalama na utulivu kwingineko. Kwa mujibu wa UNHCR watu zaidi wa 1500 wamepanda boti katika jimbo la kaskazini la Rakhine katika kipindi cha siku nne za wiki iliyopita. Kumekuwa na taarifa za watu kuzama katika mwambao wa Rakhine kmwishoni mwa wiki iliyopita lakini UNHCR imeshindwa kuthibitisha habari hizo hadi sasa na inaendelea kupata taarifa zaidi kutoka kwa serikali. Idadi ya meli na boti zinazosafiri kutoka pwani ya Bengal imeongezeka saana tangu Juni mwaka 2012 wakati kulipozuka machafuko ya kikabila kwenye jimbo la Rakhine.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031