UM wataka Sheria imara za kudhibiti makampuni binafsi ya ulinzi

Kusikiliza /

Nembo ya Umoja wa Mataifa

Serikali kote duniani zimetakiwa kutambua umuhimu wa mkataba wa kisheria wa kimataifa wa kudhibiti matumizi ya makundi binafsi ya majeshi na makampuni ya ulinzi (PMSCs) katika kusaidia mfumo wa sheria wa sasa, amesema mtaalamu huru Anton Katz ambaye anaongoza mkutano wa kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa la wanachama wa kudumu.

Bwana Katz hata hivyo amesema ulinzi ni haki ya msingi ya binadamu na jukumu nyeti la serikali lakini akasisitiza kuwa kupanuka kwa shughuli hizo za kutumiwa kwa makampuni binafsi na serikali katika usalama kunaibua changamoto kadhaa na kuhatarisha maisha ya raia na hivyo kuna haja ya kudhibiti shughuli zao.

Kadhalika mtaalamu huyo huru amesema sheria za kitaifa zilizopo haziotoshi kukabiliana na changamoto zitokanazo na utumiwaji wa makampuni binafsi katik ulinzi, kutokana na kukosekana kwa utoshelevu wa usajili wa leseni na mfumo bora wa uwazi pamoja na ulinzi dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031