UM waitaka Malaysia kuondosha marufuku ya matumizi ya neno 'Allah'

Kusikiliza /

Heiner Bielefeldt

Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Malaysia kuheshimu na kuzingatia misingi ya kidini ambayo pia inahimiza uhuru wa kuabudu kwa raia.

Wito huo umekuja kufuatana na hatua ya Malaysia kupiga marafuku waumini wa Katoliki kutumia jina la "Allah" wakimaanisha "Mungu " wakati wakiendesha ibada zao.

Mjumbe huru wa Umoja wa Mataifa juu ya uhuru wa kuabudu Heiner Bielefeldt, amesema kuwa Serikali ya Malysia inapaswa kufuta marafuku yake hiyo kwani inaweza kuchochea mvutano kutoka na makundi ya walio wachache ambao imani zao hazizingatiwi.

Amefafanua kuwa uhuru wa kuabudu ni sehemu ya msingi ya haki za binadamu na wala siyo kwa dola ama mamlaka kuchukua jukumu la kuweka masharti yanayobinya upande mmoja wa imani.

Hapo mwezi January mwaka huu, Wizara ya Mambo ya Ndani ililiamuru gazeti la Kikatoliki la Herald linalochapishwa kwa wiki mara moja kusitisha matuizi ya neno Allah ama vinginevyo lingekabiliwa na rungu la doa.Hata hivyo hatua ya serikali ya kulifungia gazeti hilo iligonga mwamba baada ya adhabu hiyo kupingwa mahakamani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930