Ugonjwa wa Kisukari umebadili maisha yangu: Mkazi wa Tanga, Tanzania

Kusikiliza /

Mkoani Morogoro Daktari akimpima Kisukari mmoja wa wakazi

Mtu anapopatiwa taarifa ya kwamba ana ugonjwa wa Kisukari, punde maisha yake hubadilika! Hulazimika kuchukua hatua kadhaa ikiwemo matibabu ya kila siku, kubadili mlo na hata mfumo wa maisha. Kama mtu alizowea mtindo fulani wa maisha hulazimika kubadili iwapo anataka kupata ahueni au kudhibiti ugonjwa huo. Shirika la afya duniani linasema hivi sasa kuna wagonjwa Milioni 350 duniani kote, na idadi itaongezeka kwa kuwa mazingira yaliyopo ni stahili kwa hilo. Mathalani vyakula vyenye mafuta mengi, watu kutokufanya mazoezi na unywaji wa vileo. Joseph Abdallah kutoka Tanzania ni mmoja wa wagonjwa wa Kisukari na katika mahojiano yake kwa njia ya simu na Assumpta Massoi wa Idhaa hii alieleza bayana maisha na ugonjwa wa Kisukari.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930