Suala la vyoo bora lasalia utata duniani, huko Ruvuma Tanzania baadhi wachukua hatua

Kusikiliza /

Tarehe 17 Novemba imetengwa kuanzia mwaka huu kuwa siku ya choo duniani. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha uamuzi huo mwezi Julai mwaka huu. Sababu hasa ni kuhakikisha suala la usafi wa vyoo na mazingira linapatiwa kipaumbele kwenye ajenda ya maendeleo endelevu. Umoja wa Mataifa unasema cha kustaajabisha ni kwamba dunia ina watu zaidi ya bilioni Saba, kati yao Bilioni Sita wana simu za mkononi lakini ni Bilioni Nne na Nusu tu wenye huduma za vyoo, tena wengi wao vyoo hivyo si salama na vinahatarisha afya zao. Je huko Tanzania hali iko vipi?

Tamimu Adamu wa Radio Washirika ya Jogoo FM mkoani Ruvuma alivinjari mjini Songea na viungani kuona hali iko vipi. Basi ungana naye kwenye makala hii ya wiki.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031