Mzozo wa Syria unachangia kuzorota zaidi hali ya usalama Iraq: Mladenov

Kusikiliza /

Baraza la Usalama(picha ya faili)

Wakati wakijitahidi kujenga taifa la kidemokrasia, kwa misingi ya utaratibu wa kisheria na ulinzi wa haki za binadamu, watu wa Iraq wanaendelea kukabiliwa na changamoto nyingi, amesema Mwakilishi wa Katibu Mkuu, na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNAMI, Nikoali Mladenov, wakati akilihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

 

Bwana Mladenov amesema changamoto kubwa zaidi ya zote ni ile ya hali ya usalama, ambayo inaendelea kuzorota.

 

"Hali hii inafanywa kuwa mbaya zaidi na mkwamo wa kisiasa, inatumiwa kwa urahisi na magaidi na makundi yenye silaha ambayo yanawalenga raia kwa nia ya kuchochea chuki za kidini, na kuidhoofisha serikali na mamlaka zilizotokana na uchaguzi. Mzozo unaoendelea sasa nchini Syria umeeneza chuki za kidini kwa ukanda mzima, na unasaidia makundi kama Al-Qaeda kujenga ushirikiano na makundi mengine yanayovuka mpaka."

 

 

 

Bwana Mladenov ameongeza kuwa changamoto za Iraq haziwezi kuzingatiwa kwa njia ya pekee, bila kuangalia matishio mengine yanayolikumba eneo zima.

 

"Kuutatua mzozo wa Syria kwa mkakati jumuishi wa kitaifa na kuridhia mkakati wa kikanda dhidi ya aina zote za misimamo mikali ya kidini na kikabila, ni muhimu katika kuleta utulivu Iraq. Hili litaweka mazingira yanayowezesha jamii zote za kikabila na kidini nchini kupata muafaka bila ushawishi kutok

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031