Mpatanishi wa mzozo wa Darfur akutana na viongozi wa Sudan Kusini

Kusikiliza /

Ibn Chambas

Mjumbe wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa ambaye ni mpatanishi wa pamoja kwa mzozo wa Darfur Mohamed Ibn Chambas, amekuwa na mazungumzo na viongozi wa Sudan Kusini ikiwa ni sehemu ya kuleta suluhu ya kidiplomasia.

Katika ziara yake nchini humo, mjumbe huyo alikutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa rais James Wani Igga, na baadaye alikutana na Waziri wa Mashauri ya kigeni na masuala ya usalama.Pande zote zilielezea namna mzozo wa eneo hilo unavyopaswa kushughulikiwa.

Kwa upande wake Chambas,alisema kuwa suluhu ya kudumu Darfur ni habari njema kwa eneo nzima na hivyo akahaidi kuendelea kuunga mkono juhudi zote za amani.

Makamu wa rais Igga alikaribisha ziara ya Chambas na kusema kuwa imekuja wakati muafaka ambako pande zote zimedhamiria kushirikiana na wapatanishi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031