Mkuu wa MONUSCO ajibu maswali ya raia wa DRC

Kusikiliza /

Mkuu wa MONUSCO Martin Kolber

Leo asubuhi, katika siku zake za kwanza kama Mkuu Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko DR Congo, MONUSCO Martin Kobler amewasiliana na watumiaji wa Intaneti na mitandao habari ya kijamii kama vile twitter, faceboook na mtandao wa Radio Okapi kujibu masuali yao kuhusu kazi anayofanya DRC. Alice Kariuki na taarifa kamili:

(RIPOTI YA ALICE KARIUK)

Akijibu masuali hayo Mkuu huyo wa MONUSCO amesema kuwa yuko DRC kuwatumikia watu wa nchi hiyo na kujenga mahusiano na watu wake wote wakiwemo vijana na wanasiasa.

Amesisitiza umuhimu wa kuwa na uwazi katika kawapa watu matumaini akisema kamwe hatatoa ahadi kuwa MONUSCO itafanya kile ambacho haitaweza kukamilisha.

Amesema Brigedi ya kuingilia kati haina suluhu za uchawi katika DRC bali suluhu ya DRC itahitaji ushirikiano na juhudi za pande zote husika zikiwemo MONUSCO, serikali, upinzani na watu wote w DRC.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930