Majanga ya wahamiaji yanamulika haja kubadili sera: ILO

Kusikiliza /

Walionusurika kifo mkasa wa Lampedusa

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Ajira, ILO, Guy Ryder, ametoa wito wa kufanywa mabadiliko ya kina katika sera za uhamiaji ili kuepukana na majanga kama yale ambayo huwaua mamia ya wahamiaji wanapjaribu kufika ulaya, wengi wao wakitoka Afrika.

Akizungumza wakati wa kongamano la siku tano la kujadili uhamiaji, likiwemo suala la haja ya kuwalinda wahamiaji, Bwana Ryder amesema anatumai kuwa majanga kama yale ambayo yamekuwa yakitokea kwenye kisiwa cha Lampedusa, Malta na hivi karibuni nchini Niger, yatamfanya kila mmoja kuzingatia zaidi haja ya kuchukua hatua.

Amesema kuna haja ya kuboresha udhibiti wa uhamiaji wa watafuta ajira kama lengo mahsusi linaloangaziwa.

Ripoti ilowasilishwa wakati wa kongamano hilo imesema wafanyakazi wahamiaji huchangia kwa kiasi kikubwa katika masoko ya ajira na chumi na jamii zao nyumbani na nchi walizohamia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930