Maelfu ya watu wahama mapigano nchini Syria na kuingia nchini Lebanon

Kusikiliza /

Wasyria wanokimbia kuelekea Lebanon (UNHCR)

Takriban watu 6000 wamekimbia makwao eneo la Qarah  nchini Syria  ambapo wamevuka mpaka na kuingia mashariki mwa Lebanon. Mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu yamekuwa nchini Lebanon tangu juma lililopita yakifanya kazi na wizara inayohusika na masuala ya kijamii kukabiliana na hali hii.

Kuhama huku kumetokana na  kuongezeka kwa ghasia eneo la Qarah na vijiji vilivyo karibu. Wale wanaohama wanasema kuwa waliishi kwenye mahandaki kabla ya kukimbia.

Wengi wa wakimbizi  wanaowasili sasa wako eneo la Arsal kaskazini mashariki mwa Lebanon. Arsal ni mji wenye wakaazi 60,000 wakiwemo wakimbizi 20,000 walioandikishwa.

UNHCR na washirika wake imefanya mipango ya kukabiliana na hali hii  ikiwa idadi hiyo itazidi kupanda. Kuna hofu kuwa  ghasia  zinazoendelea kushuhudiwa  kwenye miji ya Qarah na Qalamoun huenda zinachangia kuhama kwa watu zaidi.

Zaidi ya watu 1000 wanaowasili mji wa Arsal wamejisajili na kupewa usaidizi wanaohitaji  chakula, mablanketi, mito na vyombo vya jikoni.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031