Kuwafikia wakimbizi wa kipalestina huko Yarmouk bado ni taabu: UNRWA

Kusikiliza /

 

wakimbizi, kambini

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na usimamizi na huduma kwa wakimbizi wa kipalestina, UNRWA linazidi kupata hofu juu ya hatma ya wakimbizi hao hususan walioko kambi ya Yarmanouk kwa kuwa hivi sasa hawawezi kufikiwa ili kupatiwa huduma muhimu.

Taarifa ya UNRWA inasema wakimbizi hao wanahitaji misaada ya kibinadamu lakini kutokana na hofu ya usalama watoa huduma wanashindwa kufika. Shirika hilo linasema serikali ya Syria na pande zote husika zina mamlaka za kuwezesha UNRWA kusambaza misaada hiyo kwa usalama ili kupunguza madhila yanayokabili wakimbizi wa kipalestina. Kwa mujibu wa UNRWA tangu mwezi Julai mwaka huu licha ya maombi na jitihada kadhaa, wakimbizi wa kipalestina huko

Yarmanouk wamekuwa wakikabiliwa na fursa ndogo zaidi ya uhuru wa kutembea na hata kupata misaada ya kibinadamu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930