Kenya: Urejeshwaji wakimbizi wa Somalia utafanywa kwa hiari

Kusikiliza /

Kambi ya Dadaab, nchini Kenya

Pande zilizohusika na makubaliano juu ya wakimbizi wa Somalia walioko nchini Kenya zimesisitiza hatua ya kuwarejesha wakimbizi hao katika maeneo yao ya asili itafanywa kwa kuzingatia hiari ya mtu.

Katika taarifa yao ya pamoja, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR na serikali ya Kenya imeeleza kuwa hakuna mkimbizi atayelazimishwa kurejea nyumbani.

UNHCR imeongeza kuwa, hatua yoyote ya kuwalazimisha wakimbizi hao kurejea makwao kwa nguvu haita ungwa mkono.

Mapema Novemba 10, makubaliano ya pande tatu yaliyohusisha serikali ya Kenya, Somalia na UNHCR yalitiwa saini na hivyo kutoa fursa kwa wakimbizi hao kuwa na chaguo kuhusiana na majaliwa yao.

Makubaliano hayo yalitiwa nguvu zaidi Novemba 22 wakati makamishna wa wakimbizi kutoka serikali zote mbili walipotembelea kambi ya Daadab iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Kenya na kwa ajili ya kujadiliana mpango wa kuwarejesha wakimbizi hao.

Emanuel Nyabera ni msemaji wa UNHCR nchini Kenya

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031