Jumuiya ya kimataifa tushikamane kuwasaidia waathirika wa kimbunga Ufilipino:Amos

Kusikiliza /

Valerie Amos, OCHA azuru jamii zilizoathirika na kimbunga Haiyan, Ufilipino

Mratibu wa Umoja wa mataifa wa misaada ya dharura Bi Valarie Amos Alhamisi amezungumzia haja ya mshikamano wa jumuiya ya kimataifa kuwasaidia waathirika wa kimbunga Haiyan nchini Ufilipino.

Bi amos Jumatano alikwenda Tacloban moja ya maeneo yaliyoathirika vibaya sana na kimbunga hicho ambako amezungumza na manusura wasio na malazi , wakisubiri wa hamu msaada kuwafikia.

Amesema amejionea kwa macho athari ya kimbunga hicho kilichowaacha maelfu kwa maelfu ya watu bila makabi na kusambaratisha kabisa miundombinu. Wengi wamepoteza jamaa wa familia zao na kupingwa na bumbuazi ya kilichowasibu.

Ameongeza kuwa jukumu la jumuiya ya kimataifa hivi sasa ni kuongeza juhudi za msaada. Katika mkutano wake na Rais Benigno Aquino III na maafisa wengine wa serikali Bi amos amewahakikishia kwamba misaada ya kibinadamu itaendelea kuwafikia waathirika.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2017
T N T K J M P
« jun    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31