Jeshi la DR Congo sasa ladhibiti maeneo yote yaliyokuwa chini ya M23

Kusikiliza /

Wanawake na watoto huko Rutshuru, DR Congo wakifurahia baada ya kijiji chao kukombolewa na askari wa serikali kwa usaidizi wa MONUSCO

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko DR Congo, MONUSCO umethibitisha kuwa jeshi la nchi hiyo hivi sasa linadhibiti maeneo yote ambayo awali yalikuwa chini ya kundi la waasi la M23. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa MONUSCO iliunga mkono hatua za jeshi hilo kwa kutimiza wajibu wake wa kulinda raia.

Amesema Mkuu wa MONUSCO Martin Kobler ametaka kutumia fursa ya sasa kupatia mzozo wa DR Congo suluhu la kisiasa kwa kuendeleza mazungumzo ya Kampala ili hatimaye serikali iweze kupanua wigo wa mamlaka yake na kuleta maendeleo eneohilola nchi. Hata hivyo wametoa angalizo…

(Sauti ya Farhan)

"Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaonya vikundi vingine vya waasi visitumie ombwe la sasa la kusambaratika kwa M2, la sivyo vitachukuliwa hatua na vikosi vya MONUSCO vyenye mamlaka ya kulinda raia."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031