IOM yajiandaa kuwarejesha raia 40, 000 wa Sudan Kusini Nyumbani

Kusikiliza /

 

IOM yawarejesha waSudan Kusini nyumbani (picha ya faili)

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, limesema linajitahidi kuweza kuwarejesha nyumbani takriban raia wa Sudan Kusini 40, 000, ambao sasa wamekwama katika kambi za muda mjini Khartoum, Sudan. Taarifa kamili na Alice Kariuki.

(Taarifa ya Alice)

IOM imesema itahitaji karibu dola milioni 20 ili kuweza kuwasafirisha kwa ndege nusu ya watu hao hadi Sudan Kusini.

Watu hao wanaripotiwa kuishi katika hali ngumu, wakiwa hawana maji, huduma za usafi na makazi. Mafuriko ya hivi karibuni mjini Khartoum yaliwaathiri vibaya watu hao, na kati ya watu 48 walouawa katika mafuriko hayo, 12 walikuwa raia wa Sudan Kusini wanaosubiri kurejeshwa nyumbani katika vituo tofauti mjini Khartoum.

Raia hao wa Sudan Kusini wamekwama katika vituo hivyo kwa takriban miaka mitatu. Wengi wao waliamua kuondoka Sudan na kurudi nyumabani baada ya Sudan Kusini kujitangaza huru. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(Sauti ya Jumbe)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031