ICC yaitaka Libya imkabidhi Saif al Gaddafi kwa mahakama hiyo

Kusikiliza /

Fatou Bensouda, Mwendesha mashtaka wa ICC(Picha ya faili)

Serikali ya Libya imeombwa imkabidhi Saif al Gaddafi kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, ili afunguliwe mashtaka. Wito huo umetolewa na Mwendesha Mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda, wakati akilihutubia Baraza la Usalama kuhusu hali nchiniLibya. Joshua Mmali na taarifa kamili

TAARIFA YA JOSHUA

Bi Bensouda amesemaLibyaimepiga hatua kadhaa kisheria, ikiwemo kuridhia mkataba wa Rome, ambao uliiunda mahakama ya ICC. Amesema kuwa, ingawa kesi ya Abdallah Al-Sanousi haitakiwi tena kupelekwa kwa ICC, anataraji kuwa serikali yaLibyaitaendesha kesi dhidi yake haraka, kwa njia ya uwazi, na ambayo inaheshimu haki zake. Hata hivyo, amesema kesi dhidi ya Saif al Gaddafi bado inatakiwa kusikilizwa na mahakama ya ICC, na kuiomba serikali yaLibyaimkabidhi kwa mahakama hiyo

“Jukumu la kuwasalimisha kwenye mahakama watu ambao waranta za kukamatwa zimetolewa dhidi yao ni lazima liheshimiwe. Hisia za kisiasa hazina nafasi katika sheria, ikitumiwa kwa haki na uhuru. Natoa wito kwa serikali ya Libya kumsalimisha Saif al Gaddafi kwa mahakama ya ICC bila kuchelewa"

Bi Bensouda ametoa wito kwa Baraza la Usalama liikumbushe na kuisihi serikali ya Libya kuitikia maombi ya mahakama ya ICC, na kutoa wito kwa nchi zote wanachama ziheshimu na kutekeleza maamuzi ya majaji wa mahakama hiyo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930