Huu ni ushindi kwa Afrika, haturudi nyuma -Balozi Macharia

Kusikiliza /

Macharia Kamau

Mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa balozi Macharia Kamau amesema kile kinachoonekana kama kushindwa kwa ombi la Umoja wa Afrika kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa kwa uchunguzi na mashtaka dhidi ya viongozi wa Kenya yaliyoko Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu, ICC ni ushindi mkubwa kwa Afrika.

Katika maohjiano maalum na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza la usalama, balozi Macharia amesema Umoja wa Afrika haujakata tamaa na kwamba wana uhakika wa ushindi dhidi ya ombi lao watakaolipeleka kwenye mkitano maalum the Hague Uholanzi wiki ijayo. Akifafanua kwa msisimko hisia zake kuhusu maamuzi ya baraza la usalama balozi Kamu anaanza kwa kushangaa wanaosema Afrika imeshindwa.

(SAUTI –MAHOJIANO MACHARIA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2016
T N T K J M P
« mac    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930