Hatimaye maafikiano yafikiwa Warsaw kuhusu kupunguza gesi chafuzi

Kusikiliza /

Misitu hufyonza gesi chafuzi ya kaboni

Baada ya mijadala iloghubikwa na malumbano, hatimaye mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi mjini Warsaw, Poland umeibua fungu la maafikiano kuhusu jinsi ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi kutokana na uharibifu wa misitu.

Muafaka kuhusu kinachotajwa kama REDD+ umeungwa mkono kwa ahadi za yapata dola milioni 280 za ufadhili kutoka Marekani, Uingereza na Norway.

Rais wa mkutano huo, Marcin Korolec ameelezea fahari yake kwa mafanikio hayo ya mkutano wa Warsaw, akisema kila mmoja anafahamu mchango wa misitu wa kufyonza gesi chafuzi ya kaboni, kudhibiti tabianchi na kama maskani ya bayoanuai, lakini pia athari zitokanazo na uharibifu wa misitu kwa maisha ya watu na chumi zao.

Maafikiano yalofikiwa leo yanaweka mwongozo wa kuhakikisha mazingira yanatunzwa, na kutoa njia ya utekelezaji wa shughuli zinazohusiana na REDD+. Fungu hilo la maafikiano pia linaweka msingi wa uwazi na hadhi ya vitendo vinavyohusika na REDD+, na kudhihirisha jinsi ya kufadhili shughuli hizo na kuimarisha uratibu wa michango.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031