FAO na WHO waandaa mkutano kuhusu lishe bora

Kusikiliza /

Tatizo la lishe kwa sasa ni changamoto kwa zaidi ya nusu ya watu duniani ambapo mifumo ya chakula inatakiwa kufanyiwa mabadiliko kwa minajili ya kuboresha lishe pamoja na maisha. Haya ni baadhi ya yaliyozungumziwa wakati wa ufunguzi wa mkutano uliondaliwa na shirila la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO kwa ushirikiano na shirika la afya duniani WHO. Joshua Mmali na ripoti kamili.

(RIPOTI YA JOSHUA MMALI)

Mkutano huo wa kati ya tarehe 13 na 15 mwezi huu ni maandalizi ya mkutano wenye lengo la kuweka msingi kwa mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu lishe ambao unapangiwa kuandaliwa mwaka 2014 kuanzia tarehe 19 hadi 21 mwezi Novemba.

Lengo la mkutano huo ni kupiga jeki jitihada za kimataifa za kushughulikia masuala yakiwemo ya kilimo , kiuchumi , afya , mifumo ya afya na masuala mengine yanayohusiana na jinsi watu wanapata chakula hususan kwenye nchi zinazoendelea.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la FAO Jose Graziano da Silva anasema kuwa ni jambo lilio wazi kuwa mifumo ya sasa imeshidwa kuboresha lishe.

Jambo la kushangaza ni kwamba zaidi ya watu milioni 840 kwa sasa wanataabika kutokana na njaa hata baada ya dunia kuwa na uwezo wa kuzalisha chakula kingi kwa kila mmoja.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031