Baraza la Usalama lataka udhibiti wa vikosi vya FDLR

Kusikiliza /

Kikosi cha MONUSCO kikiwa kwenye doria huko DR Congo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeridhia taarifa ya Rais wa baraza hilo ambayo pamoja na mambo mengine inakaribisha kumalizika kwa uhasama kati ya serikali ya DR Congo na waasi wa M23 na kusema kutaka hitimisho la haraka la mazungumzo ya Kampala yanayotoa fursa ya kupokonywa silaha waasi na kuwajibika kwa waliokiuka haki za binadamu. Pamoja na kumalizika kwa uasi, taarifa hiyo imetambua kitisho kilichobakia kutoka kwa waasi wa FDLR na kusisitiza umuhimu wa kudhibiti kikosi hicho na vinginevyo vyenye silaha. Kwa mantiki hiyo wamepongeza tamko la tarehe 30 mwezi uliopita la Rais Joseph Kabila kuhusu nia ya serikali yake kudhibiti vikosi hivyo. Halikadhalika Baraza limesema linatambua na kuheshimu utaifa na uhuru wa DR Congo pamoja na nchi nyingine kwenye eneo hilo na kueleza kuwa DR Congo ina wajibu mkuu wa ulinzi wa raia, maridhiano  ya kitaifa na ujenzi wa amani na maendeleo nchini humo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930