Baraza la usalama lapongeza kazi ya kundi la kimataifa la usaidizi kwa Lebanon

Kusikiliza /

Balozi Liu Jieyi

Baraza la usalama linapongeza jitihada za kundi la ngazi ya juu la kimataifa kwa usaidizi wa Lebanon lililozinduliwa tarehe 25 mwezi Septemba mwaka huu, ndivyo ilivyoanza kauli ya Rais wa Baraza hilo Balozi Liu Jieyi alipokutana na waandishi wa habari baada ya mashauriano ya baraza hilo leo mjini New York.

Kundi analozungumzia linajumuisha Umoja wa Mataifa na mashirika yake, Umoja wa Ulaya na nchi Tano wanachama wa kudumu wa baraa la usalama ambalo jukumu lake ni kuchagiza usaidizi wa aina yoyote ambayo Lebanon inahitaji katika ujenzi wa nchi bila kusahau suala la wakimbizi wa Syria waliokimbilia nchini humo.

Balozi Li akasema kuwa baraza linasifu kasi ya kundi hilo…

"Wanachama wa Baraza wanakaribisha uhamasishaji wa kundi hili katika usaidizi wa Lebanon katika masuala ya kibinadamu, usalama, na mahitaji ya kijamii. Wamehamasisha kuendelea kwa jitihada za kutafuta kuungwa mkono kwa Lebanon. Wamesihi wananchi wa Lebanon kulinda umoja wa kitaifa wakati huu wa majaribio yanayotishia utulivu wa nchi hiyo na kusisitiza umuhimu wa kila chama kuheshimu sera ya nchi dhidi ya mgawanyiko na kuepusha kujihusisha na mzozo wa Syria na wakati huo huo kuzingatia azimio la Baabda."

Halikadhalika wametaka pande zote kushiriki kwa dhati kufanikisha kuundwa kwa serikali mapema iwezekanavyo kwa kuzingatia misingi ya demokrasia na kikatiba ya nchi hiyo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031