Baraza la usalama lalaani shambulio dhidi ya UNAMID

Kusikiliza /

Walinda amani wa UNAMID wakiwa kwenye doria

Wajumbe wa baraza la usalama wamelaani vikali shambulio la Jumapili dhidi ya walinda amani wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika waliokuwa doria huko Kabkabiya, Darfur, UNAMID, shambulio ambalo limesababisha kifo cha mlinda amani kutokaRwanda.

Rais wa baraza hilo Balozi Liu Jieyi amewaambia waandishi wa habari kuwa wajumbe wametuma risala ya rambirambi kwa familia ya mlinda amani huyo pamoja na serikali yaRwandana UNAMID huku wakitaka…

(Sauti ya Balozi Liu)

 "Wameitaka serikali ya Sudan kuchunguza haraka tukio hilo na wahusika wafikishwe mbele ya sheria. Wajumbe pia wanasisitiza uungaji wao mkono wa UNAMID na kutaka pande zote husika huko Darfur kupatia ujumbe huo ushirikiano wa kutosha."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Juni 2017
T N T K J M P
« mei    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930