Baraza la Usalama laanza harakati za kukabiliana na hali CAR

Kusikiliza /

Jan Eliasson

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamefanya maziungumzo leo Jumatatu jioni na kukubaliana kuwa kuna haja ya kuanza harakati za kukabiliana na hali ya usalama inayozidi kuzorota katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao hicho ambacho baadaye kilifanywa faraghani, Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson amesema amezingatia muungano wa mawaidha kuhusu kukabiliana na hali hii hatari sana, ambapo kuna ghasia za mara kwa mara na ambazo zimeenea, na huenda zikabadilika kuwa janga kubwa.

"Hatari hii imeghubika mazungumzo ambayo tayari tulizungumzia katika ripoti ya Katibu Mkuu wiki ilopita. Tunatajia kuwa sasa kutakuwa na hatua ya haraka. Siyo suala la kutoa tahadhari ya mapema tena, kwani tumekuwa na hali hiyo kwa muda sasa, na suala sasa ni kuitikia hali hiyo kwa kuchukua hatua mapema.

Katika muktadha huo, Ufaransa imepewa jukumu la kuandaa mswada wa azimio la kukabiliana na hali hiyo hatari ya usalama katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwanza kwa kutoa msaada kwa wanajeshi wapatao 3,000 wa Muungano wa Afrika ambao tayari wapo CAR, ili idadi iongezwe hadi 3,600, na kusaidia harakati za kisiasa za mpito.

Mwakilishi wa Ufaransa amesema huenda azimio hilo pia litaidhinisha kuundwa kwa kikosi cha kulinda amani katika nchi hiyo. Lakini ili kufanya hivyo, Katibu Mkuu ameombwa kuwasilisha ripoti kwa Baraza hilo, itakayokariri haja ya kuundwa kikosi hicho cha kulinda amani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031