Ban awasili Mali katika mwanzo wa ziara yake Sahel

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon na Rais wa Bank ya dunia Jim Yong Kim wamewasili Bamako Mali katika mwanzo wa ziara ya pamoja huko Sahel. Grace Kaneiya na maelezo zaidi

(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

Katika ziara hiyo ya pamoja viongozi hao watazuru pamoja na Mali, Niger, Burkina Faso na Chad. Walipowasili Bamako Katibu Mkuu amezungumza na waandishi wa habari kuelezea kwanini yeye na viopngozi wengine wa dunia wanakwenda katika ukanda wa Saheli pamoja. Andre Michel ameambatana na Katibu Mkuu katika ziara hiyo

(SAUTI YA ANDRE MICHEL)

Ban na Yong Kim wamewasili Mali wakati ambapo miili ya waandishi wawili wa Kifaransa waliouawa siku mbili zilizopita ikiandaliwa kwa safari ya kurejeshwa nyumbani. Akizungumzia Ban alichosema kuhusu mauaji hayo Andre Michel amesema

(SAUTI YA ANDRE MICHEL)

Baada ya kutoka Mali Ban na Rais wa Bank ya dunia wataelekea Niger.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930