Ban asifia mazungumzo ya amani Colombia

Kusikiliza /

KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amekaribisha tangazo lililofanywa jana na serikali ya Colombia na Kundi lililojihami la mapinduzi la FARC kuwa wamefikia makubaliano kuhusu kushirikishwa kisiasa kwa kundi hilo, katika mazungumzo yanayoendelea mjini Havana, Cuba.

Kwa mujibu wa taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban ametilia mkazo umuhimu wa uaminifu na mbinu za kuhakikisha kuwa umma unashirikishwa katika kutafuta amani ya kudumu, kwa misingi ya demokrasia na heshima ya haki za binadamu. Amezisifu pande husika kwa kujitoa kutekeleza makubaliano hayo, huku zikizingatia jinsia na ujumuishaji wa wanawake katika harakati za kisiasa.

Katibu Mkuu amekaribisha tangazo kuwa mazungumzo yataendelea mjini Havana, na kuwatakia wajumbe wanaoshiriki ufanisi katika kufikia makubaliano kuhusu masuala yalosalia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930