Ban amteua Juan Somavia kuwa Mshauri wake kuhusu ushirikiano wa kikanda kuhusu sera

Kusikiliza /

Juan Somavia ILO

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Bwana Juan Somavía wa Chile kuwa Mshauri wake Maalumu kuhusu ushirikiano wa kikanda kuhusu sera.

Bwana Somavía ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ajira, ILO, atasaidia kuweka mkakati wa miaka miwili wa ushirikiano wa kisera kuhusu masuala fulani muhimu miongoni mwa tume za kikanda za Umoja wa Mataifa, kwa misingi ya mambo yanayoendelea kutekelezwa, na kuchangia katika kuwezesha mikakati ya kikanda ya ushirikiano wa kisera. 

Bwana Somavía atatekeleza wajibu huo katika ofisi za Tume ya Kiuchumi ya Nchi za Amerika ya Kusini na Karibea mjini Santiago, Chile. Alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa ILO kutokea 1999 hadi 2012. Kabla ya hapo, aliwahi kuhudumu kama Mwakilishi wa Kudumu wa Chile kwenye Umoja wa Mataifa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031