Ban alaani mashambulizi huko Lebanon

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameshutumu vikali shambulio la kigaidi lililotokea leo karibu na ubalozi wa Iran uliopo mji mkuu wa Lebanon, Beirut na kusababisha vifo vya raia 23 akiwemo mwanadiplomasia mmoja wa Iran na majeruhi zaidi ya mia moja. Ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za waliokufa pamoja na serikali ya Lebanon na ile ya Iran huku akiwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa Lebanon kutambua kuwa mashambulizi ya aina hiyo na ya kuchukiza yanalenga watu wote na kutaka pande zote nchini humo kuchukua hatua za kujizuia na kuunga mkono mamlaka za dola hususan vyombo vya usalama katika kuzuia matukio zaidi ya ugaidi. Katibu mkuu amesema ni matumaini yake kuwa wahusika wa shambulio hilo watafikishwa mbele ya sheria haraka iwezekanavyo na kusisitiza azma ya jumuiya ya kimataifa ya kusaidia utulivu na usalama nchini Lebanon.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031