Ban akutana na Waziri Mkuu wa Poland

Kusikiliza /

KM Ban na Waziri Mkuu wa Polanda, Donald Tusk

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Polanda, Donald Tusk, pembezoni mwa mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, ambayo yanaendelea nchini humo katika mji mkuu, Warsaw.

Katika Mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, Bwana Ban na Waziri Tusk wamejadili kuhusu jinsi ya kuimarisha zaidi ushirikiano uliopo kati ya Poland na Umoja wa Mataifa, na kuipongeza Poland kwa mchango wake kwa Umoja wa Mataifa, kama taifa ambalo mfano wake wa kufanikiwa kujikwamua kisiasa na kiuchumi unaweza kuigwa na mataifa mengine.

Viongozi hao wawili pia wamejalijadili suala la mzozo wa Syria, ambapo Bwana Ban ameutaja mkutano wa kidiplomasia anaouandaa kuhusu nchi hiyo kama matumaini ya mwanzo wa kikomo cha mapigano.

Pia wamegusia janga la hivi karibuni Ufilipino, na lile la kimbunga hapo jana huko Sardinia, Italia, pamoja na suala zima la mabadiliko ya tabianchi. Bwana Ban amesema wote wanatambua kuwa ushirikiano unahitajika katika kukabiliana na suala la mabadiliko ya tabianchi, kwani linamuathiri kila mmoja.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031