Ban aitaka Burkina Faso kupambana na mabadiliko ya tabia nchi

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akiwa na Waziri Mkuu wa Bukirna Faso Luc-Adolphe Tiao

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon akiwa angali ziarani katika ukanda wa Sahel amekutana na kuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu Luc-Adolphe Tiao na baraza la mawaziri la Burkina Faso ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia mabadiliko ya tabianchi kama miongoni mwa changamoto kuu zinazoikumba nchi hiyo na kutaka nguvu za pamoja katika kukabiliana na mabadiliko hayo.

Bwana Ban amesema lazima kuwa na mkakati wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo amesisitiza husababishwa na binadamu.

Ripoti ya tano ya jopo la kimataifa la mabadiliko ya hali ya hewa, IPCC imeweka wazi kuwa mabadilko ya tabinchi yanatokea kwasababu yenu, kwasababu ya binadamu, kwasababu yetu. Hatuwezi kulaumu asili, tunachoweza kufanya ni kujilaumu sisi wenyewe. Kwa hiyo ni muhimu kwamba tuamue kuwa na makakati

Kadhalika Katibu Mkuu Ban amezungumzia utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia kwa kuwasihi viongozi wa Bukina Faso kutumia utashi wa kisiasa pamoja na rasilimali ili kutimiza malengo hayo kabla ya amwaka 2015.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930