Bado tunajadili orodha rasmi ya washiriki:Brahimi

Kusikiliza /

Jeffrey Feltman, Mkuu wa masuala ya Siasa ndani ya Umoja wa Mataifa akiwa na Lakhdar Brahimi mjini Geneva

Baada ya kutangazwa kuwa tarehe 22 ya mwezi Januari mwakani ni siku ya kufanyika kwa mkutano wa pili wa amani kuhusu Syria huko Geneva, mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na nchi za kiarabu juu ya mzozo wa Syria, Lakhdar Brahimi amesema wanachofanya sasa ni kujadili orodha kamili  ya washiriki. Amewaambia waandishi wa habari kuwa kikao cha mwisho cha utatu kikihusisha Umoja wa Mataifa, Urusi na Marekani kitafanyika tarehe 20 mwezi ujao.

(Sauti ya Brahimi)

"Tunafanya mawasiliano na serikali na upande wa upinzani watujulishe majina ya wajumbe washiriki wao kabla ya mwisho wa mwaka huu na ni vyema tukutane nao. Mkutano ni fursa kwa wasyria kuja Geneva kuzungumza baina yao na kujenga mchakato wa amani unaotekelezeka kwa ajili ya nchi yao.

Bwana Brahimi amesema mchakato huo ni endelevu na si kila mtu anayetaka kushiriki ataweza kufanya hivyo na kwamba yeyote anayetaka kujengaSyriaatafanya hivyo kupitia mchakato huo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031