Nyumbani » 29/11/2013 Entries posted on “Novemba 29th, 2013”

Ban akaribisha tamko la baraza la usalama kuhusu Yemen

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha tamko la baraza la usalama la tarehe 27 November ambalo limeahidi kusaidia katika mchakato wa amani wa mpito nchiniYemen ikiwamo kongamano la mjadala wa kitaifa. Katibu Mkuu amesema baraza hilo linaendelea kusikitishwa na kuingiliwa au kucheleweshwa machakato wa mpito na kwamba baraza hilo liko tayari kuzingatia [...]

29/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Umuhimu wa televisheni ni zaidi ya kuhabarisha nchini Burundi

Kusikiliza / Televisheni

Televisheni au kwingineko ikijulikana kama Runinga imeleta mabadiliko makubwa katika mtazamo wa vipindi hususan kwenye nchi ambazo awali radio ilikuwa imeshika kasi. Televisheni ina umuhimu wake katika kuhabarisha, kuelimisha na hata kuburudisha na ndio maana tarehe 21 ya mwezi Novemba imetengwa kuwa siku ya televisheni duniani. Hata hivyo maadhimisho ya nyakati hizo yanakuja na mengi [...]

29/11/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

MINUSMA yalaani ghasia huko Kidal nchini Mali

Kusikiliza / Moja ya vituo vya ukaguzi huko Kidal nchini Mali

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchiniMali, MINUSMA umeshutumu vikali ghasia za karibuni huko Kidal kaskazini mwa nchi hiyo na kutaka pande zote husika kujizuia. Ghasia hizo za Alhamisi zimetokea licha ya mpango wa ulinzi wa ujulikanao kama Serval ambao unaratibiwa kwa pamoja na serikali ya Mali na MINUSMA kwa  usaidizi wa Ufaransa. [...]

29/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama bado ni tete CAR; Mia Farrow ashuhudia

Kusikiliza / Mia Farrow akizungumza na wakazi wa CAR wakiwemo watoto

Huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, hali ya usalama inazorota lakini juhudi za Umoja wa Mataifa zinaendelea ili kusaidia waathirika wa mgogoro unaondelea nchini humo. Juhudi za hivi karibuni zaidi ni ziara ya balozi mwema wa shirika la Umoja UNICEF Mia Farrow aliyefika CAR kuanagalia athari za mgogoro. Ungana Na Joseph Msami katika makala [...]

29/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban aziomba nchi wanachama kuunga mkono watu wa Palestina

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameziomba nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuunga mkono juhudi za utafutaji suluhu la mataifa mawili ili kuutokomeza mgogoro kati ya Israel na Palestina. Bwana Ban amesema hayo katika ujumbe wake wa Siku ya Kimataifa ya kusimama bega kwa bega na watu wa Palestina, ambayo ni [...]

29/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Yemen yakiuka mkataba unaopiga marafuku silaha za ardhini

Kusikiliza / Utafiti wa silaha ardhini

Yemen imekiri kuwa imekwenda kinyume na mkataba wa kimataifa unaopiga marafuku matumizi, kuhifadhi na kuzalisha kwa silaha za ardhini. Kampeni ya kimataifa inayopiga marafuku silaha za ardhini imesema kuwa iliitaka serikali ya Yemen kuondosha maelfu ya silaha mwaka 2011 katika baadhi ya sehemu mbili. Kujitokeza kwa machafuko ya kiraia katika miaka ya hivi karibuni ni [...]

29/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa UM kuchunguza hali ya watu wenye asili ya Afrika Brazil

Kusikiliza / Watu wenye asili ya Afrika Brazil

Kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye asili ya Afrika litafanya ziara ya siku kumi nchini Brazil, kuanzia Disema 3 hadi 13 2013, ili kuchunguza masuala kadhaa yanayohusu haki za binadamu za watu wenye asili ya Afrika nchini humo. Mmoja wa wataalamu hao, Mireille Fanon-Mendes-France amesema kuwa Brazil imepiga hatua nyingi katika [...]

29/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini yazindua ushirika wa kulinda haki za watoto

Kusikiliza / Watoto wakiwa darasani kwenye shule moja huko Juba, Sudan Kusini

Shirika la Kuhudumia watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limeipongeza serikali ya Sudan Kusini kwa kuanzisha shirikisho la wadau wa kulinda haki za watoto walio hatarini, ambalo ni la kwanza la aina yake nchini humo. Mwakilishi wa UNICEF nchini humo, Iyorlumun Uhaa, amesema kuwa watoto maskini zaidi na walio wanyonge zaidi katika nchi yoyote ile huwa [...]

29/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Virusi vya MERS Corona vyabainika kwa ngamia Qatar:WHO

Kusikiliza / Ngamia waripotiwa kuwa na virusi vya MERS Corona huko Qatar

Shirika la afya duniani WHO litatoa ripoti ya uchunguzi kutoka Qatar inayoashiria kuwepo kwa virusi vya MERS Corona miongoni mwa ngamia. Shirika hilo linasema hii ni mara ya kwanza ngamia kuambukizwa virusi vya corona nchini humo lakini njia ya kuambukizwa kwao bado ni kitendawili. Matokeo ya utafiti huo kwa mujibu wa WHO yanatoa mwangaza wa [...]

29/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wakimbizi kutoka Syria wanabiliwa na wakati mgumu siku za baadaye: UNHCR

Kusikiliza / Watoto wa Syria

Watoto wa wakimbizi walio nchini Lebanon na Jordan wanakabiliwa na wakati mgumu siku za baadaye huku wakiwa wanalazimika kufanya kazi kutafutia familia zao au wakiwa wanalazimishwa kujiunga na makundi yaliyojihami kwa mujibu wa  shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa. Utafiti uliofanywa kwa watoto wa wakimbizi wa Syria kwenye nchi za Lebanon na Jordan [...]

29/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini yazidi kutekeleza hukumu ya kifo hata baada ya kutia sahihi makubaliano ya UM

Kusikiliza / Hukumu ya kifo bado inatekelezwa Sudan Kusini

Ofisi ya haki za bindamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa watu wanne wamenyongwa nchini Sudan Kusini huku wengine 200 wakiwa kwenye  orodha ya kusubiri kunyongwa. Jason Nyakundi na taarifa kamili. (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) Kulingana na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ni kuwa idara ya mahakama nchini Sudan Kusini inakabiliwa [...]

29/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya walioathirika na kimbunga Haiyan sasa ni zaidi ya milioni 14:OCHA

Kusikiliza / Athari za Kimbunga Haiyan, Ufilipino

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kiutu OCHA linasema kuwa idadi ya watu walioathirika na kimbuka Haiyan nchini Ufilipino imezidi kupindukia. Kwa mujibu wa OCHA, zaidi ya watu milioni 14.4 wameathiriwa na kimbunga hicho ambapo kati yao, milioni 3.62 wamekosa makazi, milioni 1.1 nyumba zao zimebomolewa na vifo vilivyoripotiwa hadi sasa vimefikia [...]

29/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maambukizi mapya ya Ukimwi yapungua: UNAIDS

Kusikiliza / Moja kliniki za kutoa huduma dhidi ya Ukimwi kwa mama na mtoto nchini Lesotho

Wakati dunia inaelekea kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani tarehe Mosi Disemba, habari njema ni kwamba idadi ya maambukizi mapya ya virusi vinavyosababisha Ukimwi imepungua. Taarifa hizo zimo kwenye ujumbe wa siku hiyo uliotolewa na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na vita dhidi ya Ukimwi, UNAIDS Michel Sidibé. Katika ujumbe huo wa [...]

29/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vifo vya raia wa Haiti katika pwani ya Bahamas vitupe funzo:IOM

Kusikiliza / Nembo ya IOM

Vifo vya wazamiaji 30 wa Haiti waliokumbwa na umauti wakati wakiwa safarini katika ufukwe wa Bahama mapema wiki hii kumezidi kuongeza hali ya wasiwasi kuhusiana na wimbi la wahamiaji haramu wanaokwenda katika nchi za mbali huku wakitumia mashua zisizo na usalama. Kwa mujibu wa shirika la kimataifa linalohusika na wahamiaji IOM, kuna hali ya kutia [...]

29/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP inaendelea kuongeza misaada CAR:

Kusikiliza / Chakula

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linaendelea kuongeza operesheni za kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati licha ya hali kuzidi kuwa mbaya.  Shirika hilo limeshasambaza msaada wa chakula kwa maelfu ya watu mjini Basonga lakini limesema watu takribani milioni 2.9 wanahitaji msaada wa kibinadamu nchini humo. Hivi karibuni tani 358 za chakula [...]

29/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM yaomba dola milioni 10 kuwarejesha Wasouth Sudan kwao

Kusikiliza / WaSudan Kusini warejeshwa nyumbani na IOM

Shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM linaomba dola milioni 10.5 ili liweze kutoa msaada wa dharura wa kuwarejesha watu wasiojiweza wa Sudan Kusini kwao. Watu hao wamekwama mjini Khartoum Sudan kwa muda sasa. IOM inasema watu hao hawana uwezo na njia yoyote ya kuwarejesha nyumbani Sudan Kusini. Shirika hilo limeongeza kuwa watu hao wamekuwa wakiishi [...]

29/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lalaani vikali shambulio dhidi ya ubalozi wa Urusi Damascus:

Kusikiliza / Baraza la usalama

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamesikitishwa na kulaani vikali shambulio la magruneti dhidi ya ubalozi wa Urusi mjini Damascus Syria siku ya Alhamisi. Shambulio hilo limekatili maisha ya mtu mmoja na kujeruhi wengine 9 wakiwemo walinzi wa ubalozi huo. Wajumbe hao wametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulio [...]

29/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031