Nyumbani » 27/11/2013 Entries posted on “Novemba 27th, 2013”

Twaunga mkono mchakato wa kisiasa Yemen, pande ziharakishe ukamilike: Baraza

Kusikiliza / Balozi Liu Jieyi

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wametoa ujumbe wa pamoja na ulio dhahiri ambao unaunga mkono mchakato wa kisiasa unaoendelea nchini Yemen pamoja na jitihada za serikali ya nchi hiyo za kujenga upya uchumi, kuimarisha usalama ikiwemo mjadala wa kitaifa. Msimamo huo umeelezwa kwa waandishi wa habari na Rais wa Baraza hilo [...]

27/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na kusambaa kwa ghasia Misri

Kusikiliza / Ramana ya Misri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anasikitishwa na hatua ya kuwekwa vizuizini, na kusambaa kwa ghasia za waandamanaji nchini Misri ikiwamo taarifa za mashambulio ya kijinsia. Katika taarifa yake iliyotolewa mjini New York Bwana Ban amesisitiza umuhimu wa kuheshimu maaandamano ya amani na uhuru wa kukusanyika ikiwa ni pamoja na mazungumzo na [...]

27/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Masaibu ya wakimbizi wa Syria walioko Lebanon yaangaziwa

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria walioko Lebanon

Siku chache baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza tarehe 22 January mwakani ya kufanyika kwa mkutano wa pili wa amani kuhusu Syria huko Geneva, wakimbizi wa nchi hiyo walioko katika kambi nchini Lebanon wanaelezea madhila wanayokutana nayo. Hapa katika mji wa Arsal nchiniLebanonkuna foleni kubwa ya watu nje ya kituo cha usajili. Zaidi ya familia [...]

27/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban na Kim wazungumzia nishati endelevu

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim

Ilikufanikisha malengo ya nishati endelevu kwa wote ni muhimu kukuza uwekezaji mkuu na wa ziada amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Akiwa ameambatana na rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York kufuatia kikao cha ngazi ya juu cha bodi ya mpango wa nishati [...]

27/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM wataka hatua zichukuliwe haraka baada ya ripoti za mauaji ya watoto Kinshasa :

Kusikiliza / Mama na mwanawe waliyefurushwa asimama katika kambi ya Mugunga picha ya MONUSCO

Umoja wa Mataifa leo umetoa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuchukua hatua haraka kufuatia ripoti za kusikitisha  za kupotea na kuuawa kwa watoto na vijana yaliyokwenda sanjari na operesheni ya serikali ya kukabiliana na uhalifu mjini Kinshasa. Kwa mujibu wa ripoti ambazo kwa sasa zinathibitishwa na watu 20 wakiwemo watoto 12 [...]

27/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa UM Yemen azuru Sa'ada:

Kusikiliza / Wakimbizi wa Yemen

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed, amezuru mji wa Sa'ada Kaskazini mwa Yemen na kukutana na gava, tume ya rais, tume ya bunge, viongozi wa eneo hilo na  wadau wengine wa misaada ya kibinadamu. Ziara yake imekuja wakati ambapo machafuko kwaskazini mwaYemenhususan Dammaj na Kitaf yameingia [...]

27/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Serikali ziweke mipango ya maendeleo ya kupunguza majanga:ESCAP

Kusikiliza / Kimbunga Haiyan Ufilipino, mfano wa janga

Kujenga uwezo mkubwa wa kukabiliana na majanga katika eneo la Asia-Pacifiki ndio ajenda kuu kwenye mkutano wa siku tatu ulioanza Jumatano katika tume ya Umoja wa Mataifa ya kiuchumi na kijamii kwa nchi zaAsiana Pacific ESCAP.Taarifa ya Flora Nducha inaarifu  (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)  Mkutano huo unaofanyika mjini Bangkok Thailand umewaleta pamoja maafisa wa serikali [...]

27/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya jitihada China yahiizwa kuhifadhi mazingira:UNEP

Kusikiliza / Mazingira China

Licha ya juhudi za China za kukuza uchumi unaolinda na kuhifadhi mazingira taifa hilo bado linakabiliwa na changamoto za kimazingira na kijamii ambazo lazima zishughulikiwe iwapo nchi hiyo inalenga kwa dhati kutimiza malengo endelevu ya maendeleo. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyotolewa wiki hii na wizara ya uhifadhi wa mazingira nchini China, [...]

27/11/2013 | Jamii: Rio+20, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Global Fund yapigwa jeki kwa dola milioni 46 kupitia uuzaji wa mnada

Kusikiliza / Nembo ya Global Fund

Mfuko wa Global Fund kwa ajili ya kupambana na malaria, kifua kikuu na HIV umepigwa jeki kwa mchango wa dola milioni 46, zilizotokana na zoezi la uuzaji wa mnada lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Renew, Energize and Donate (RED), pamoja na michango mingine. Joshua Mmali na taarifa kamili.   (TAARIFA YA JOSHUA) Zoezi [...]

27/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yapitisha idadi ya wakimbizi wa Ivory Coast iliowarudisha nyumbani kutoka Liberia

Kusikiliza / Wakimbizi wa Ivory Coast wakielekea nyumbani kutoka Liberia

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR  Iemepitisha idadi ya wakimbizi  wa Ivory Coast lililowarudisha nyumbani kwa hiari kutoka  nchini Liberia ikiwa pia na mipango ya kuwarudisha  nyumbani wakimbizi zaidi kabla ya mwisho wa mwaka huu. Jason Nyakundi na ripoti kamili.(Taarifa ya Jason) Hadi mwishoni mwa juma lililopita UNHCR ilikuwa imewasaidai wakimbizi 16,232 [...]

27/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada wa haraka wahitajika kwa wakulima Ufilipino: FAO

Kusikiliza / Moja ya shamba la kuku ambalo limesambaratishwa na kimbunga Haiyan

Kimbunga Haiyan kimesababisha madhara makubwa nchini Ufilipino lakini madhara hayo yanaweza kuwa maradufu zaidi kwa wakulima iwapo hatua hazitachukuliwa kuwapatia usaidizi wa kuwawezesha kuendelea na kilimo kwa ajili ya kujipatia kipato. Hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO ambalo linatoa wito kwa mashirika ya utoaji misaada kuchukua hatua za haraka [...]

27/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mpatanishi wa Darfur akutana na rais wa Chad

Kusikiliza / Mohammed Ibn Chambas

Kiongozi wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwa mzozo wa Darfur nchini Sudan Mohamed Ibn Chambas amekutana na Rais wa Chad Idriss Derby katika kile kinachoelezwa kwamba ni jaribio la kidiplomasia la kufanikisha mazungumzo ya amani ya Darfur. Msuluhishi huyo wa kimataifa anayeongoza UNAMID ametoa picha halisi ya usalama [...]

27/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WHO yatoa mwongozo mpya wa kutibu watoto wenye unyafuzi

Kusikiliza / Mtoto akipimwa mzunguko wa mkono kufahamu iwapo na utapiamlo

Shirika la afya duniani, WHO leo limetoa mwongozo mpya wa tiba kwa watoto wenye unyafuzi au utapiamlo uliokithiri unaoripotiwa kuwa tatizo kubwa kwa watoto Milioni 20 duniani kote wenye umri wa chini  ya miaka mitano. George Njogopa na ripoti kamili. (Ripoti ya George) WHO inasema kuwa hali mbaya ya utapiamlo inajitokeza wakati ambapo mtoto anakuwa [...]

27/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031