Nyumbani » 22/11/2013 Entries posted on “Novemba 22nd, 2013”

Hatimaye maafikiano yafikiwa Warsaw kuhusu kupunguza gesi chafuzi

Kusikiliza / Misitu hufyonza gesi chafuzi ya kaboni

Baada ya mijadala iloghubikwa na malumbano, hatimaye mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi mjini Warsaw, Poland umeibua fungu la maafikiano kuhusu jinsi ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi kutokana na uharibifu wa misitu. Muafaka kuhusu kinachotajwa kama REDD+ umeungwa mkono kwa ahadi za yapata dola milioni 280 za ufadhili kutoka Marekani, Uingereza na Norway. Rais wa [...]

22/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kampeni ya chanjo kwa watoto Ufilipino kuanza Jumatatu: OCHA

Kusikiliza / Watoto hawa wako hatarini kuambukizwa magonjwa

Hivyo ndivyo Mkuu wa ofisi ya masuala ya usaidizi wa kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, Valerie Amos alipoanza mkutano wake na waandishi wa habari mjini New York, akieleza kile alichoshuhudia huko Ufilipino baada ya kimbunga Haiyan kupiga nchi hiyo na kusababisha vifo na majeruhi pamoja na kupoteza makazi. Bi. Amos ambaye amekwenda Ufilipino mara mbili [...]

22/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNFCCC yazindua ubia mpya na kampuni ya GeSI

Kusikiliza / UNFCCC-LOGO

Makubaliano kati ya taasisi ya Umoja wa Mataifa inayosimamia mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa, UNFCC na kampuni ya kimataifa ya suluhu endelevu mtandaoni, GeSi yanalenga kutafuta na kueneza matumizi ya teknolojia zisizo na madhara kwa mazingira. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya pande mbili hizo ikikariri UNFCCC ikisema [...]

22/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukatili wa kingono wapigwa vita nchini Kenya

Kusikiliza / Maafisa wa Kenya katika usaidizi

Wakati dunia ikiadhimisha mkataba wa watoto unaolinda haki za kundi hilo muhimu katika jamii, nchini Kenya, kama kwingineko duniani, visa vya ubakaji vinatajwa. Hata hivyo katikati ya wingu hilo la ukatili wa kingono kuna habari njema za kuwanusuru wahanga wa matuko hayo. Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo .

22/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

IOM yawakwamua wahamiaji wasio na nyaraka toka Tanzania walio mipakani huko Maziwa makuu

Kusikiliza / Jumbe Omari Jumbe, msemaji wa IOM

Taarifa zinasema maelfu ya wahamiaji kutoka Tanzania wamekwama mipakani huku hali ya wasiwasi juu ya majaliwa yao ikiibuka. Hii inafuatia zoezi la serikali ya Tanzania kuwaondoa wahamiaji hao katika zoezi lililotangazwa na kutekelezwa na serikali hiyo. Hivi karibuni. Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limejikita kuwasaidia wakimbizi hao kama msemaji wa shirika la uhamiaji IOM [...]

22/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Wigo wa vyanzo vya ajira upanuliwe: Dkt. Kituyi

Kusikiliza / Kijana akijaribu kujipatia kipato

          Wiki hii Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo, UNCTAD limetoa ripoti kuhusu nchi zenye maendeleo duniani, LDCs kauli mbiu ikiwa  ustawi na ajira kwa maendeleo jumuishi na endelevu. Nchi hizo ziko 48 na miongoni mwao 34 zinatoka Afrika ikiwemo Burundi, Rwanda, Uganda na Tanzania. Je ni mambo [...]

22/11/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili wa kingono haukubaliki, bila kujali kavalia nini mwanamke: Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kaatika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amesema  kila mmoja anatakiwa kutimiza jukumu lake la kukomesha imani zinazosaidia kuendeleza mazingira ambayo yanafanya ukatili dhidi ya wanawake kuonekana kama jambo la kukubalika, au kwamba wanawake hao wanastahili kufanyiwa ukatili. Amesema ukatili wa kingono hauwezi kukubalika kamwe, bila kujali mwanamke kavalia nini. [...]

22/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IUCN yachukua hatua kudhibiti biashara haramu ya ngozi ya Chatu

Kusikiliza / Nyoka

Hofu juu ya kutoweka kwa aina kuu mbili za chatu Kusini Mashariki mwa Asia kumesababisha kuanzishwa kwa ubia kati ya shirika la kimataifa la uhifadhi, IUCN na kampuni ya KERING inayomiliki nembo ya GUCCI. Ubia huo ulioanzishwa na kituo ha kimataifa cha biashara, ITC unalenga kuhakikisha biashara endelevu ya ngozi ya nyoka huyo aina ya [...]

22/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi zaidi wa Syria wakimbilia Lebanon

Kusikiliza / syrian refugees Lebanon

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa zaidi ya familia 500 za Syria zimelazimika kuvuka mpaka siku ya jumatano usiku na kukimbilia eneo la Aarsal kutokana na kuenea kwa mapigano hadi katika maeneo ya Nabek na Yabroad. Shirika hilo linasema kuwa zaidi ya watu 10,000 wamepatiwa msaada wa chakula. Idadi ya wakimbizi walioandikishwa [...]

22/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM yachukua hatua ya kuwalinda manusura kutoka mikononi mwa wasafirishaji haramu wa watu

Kusikiliza / Manusura wa Kimbunga Haiyan

Huku watu zaidi wakijaribu kuhama maeneo yaliyokumbwa na kimbunga Haiyan nchini Ufilipino shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na serikali ya Ufilipino na washirika wake wamekuwa wakifanya jitiha za kuwazuia wale wanaohama kutoka kwa wasafirishaji haramu wa watu na kutambua mahitaji ya watu hao. IOM inakadiria kuwa hadi watu 5000 wanakimbia maeneo yaliyoathiriwa [...]

22/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wasio na vibali wakwama mipakani huko Maziwa makuu; IOM yatoa usaidizi

Kusikiliza / Burundian refugees

Wakati idadi kubwa ya wahamiaji wasiokuwa na vibali ambao hivi karibuni walifukuzwa nchini Tanzania wakiendelea kukwama katika maeneo ya mipakani, kumezuka hali ya wasiwasi juu ya majaliwa hayo.  Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, limesema wahamiaji hao kutoka nchi za Rwanda, Uganda na Burundi wapo katika hali mbaya kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika [...]

22/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa DRC waanza kurejea nyumbani kutoka Uganda

Kusikiliza / DRC refugees

Takriban wakimbizi elfu saba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliotorokea nchi jirani ya Uganda kufuatia makabiliano kati ya jeshi la serikali ya DRC na waasi wa M23, wamerejea makwao baada ya utulivu kurejea. John Kibego wa redio washirika ya Spice FM, ana ripoti kamili kutoka Uganda. (Tarifa ya John Kibego) Wakimbizi 3,275 pekee ndio [...]

22/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto 6000 vitani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati: UNICEF

Kusikiliza / car-violence

Kundi moja lililojihami nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati limewaingiza karibu watoto 6000 kwa jeshi lao kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi. (Taarifa ya Jason) Karibu nusu ya watoto hao wameingizwa jeshini mwaka huu kufuatia kupinduliwa kwa serikali na waasi mwezi nMachi. UNICEF inasema [...]

22/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa Polio waanza kudhibitiwa eneo la Pembe ya Afrika

Kusikiliza / Polio-Horn-Africa-1Web

Kumekuwa na mafanikio ya kukabiliana na ugonjwa wa kupooza uliolipuka katika eneo la pembe ya Afrika miezi sita iliyopita ambao uliathiri watoto kiasi cha 2000 na watu wazima kadhaa. Maeneo yaliyopigwa na ugonjwa huo ni pamoja na Somalia, Kenya na Ethiopia. Ripoti zinaonyesha kuywa maeneo mengi yaliyokumbwa na tatizo hilo sasa yameanza kupata afuani kutokana [...]

22/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa OCHA ahitimisha tathmini ya janga la kimbunga huko Ufilipino

Kusikiliza / Valerie Amos ziarani Ufilipino

Mkuu wa Ofisi ya masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa, OCHA, Bi. Valerie Amos amehitimisha tathmini yake ya usaidizi wa kibinadamu huko Ufilipino kufuatia janga la kimbunga Haiyan lililopiga nchi hiyo takribani wiki mbili zilizopita. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi. (Taarifa ya Assumpta) Baada ya ziara ya wiki hii kwenye maeneo ya Tacloban, [...]

22/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031